Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Phiri akutana na mabosi Simba

Muktasari:

  • Simba ipo katikati ya mtihani mzito wa kuachana na mshambuliaji wao Mosses Phiri ambaye anatajwa kujiunga na Yanga, Azam na Singida Fountain Gate.

Dar es Salaam. Mabosi wa Simba wamekutana na mshambuliaji wake Mosses Phiri kutazama namna ya kusitisha mkataba kwa pande hizo mbili.

Simba inataka kuachana na Phiri kwenye dirisha hili la usajili linalofungwa leo usiku Januari 15, 2024 ikikabiliwa na kusaka nafasi ya kutumia nafasi ya mchezaji mpya wa kigeni kati ya wawili waliosajiliwa.

Pande hizo mbili zikiwa mezani Simba imeleta hoja ya kumtoa kwa mkopo mshambuliaji huyo Mzambia akacheze nje ya nchi atakapochagua.

Hoja hiyo ya Simba pia inalenga kumkwamisha mshambuliaji asielekee kwa wapinzani wao Yanga, Singida, Ihefu na Azam ambao wanavizia huduma ya Mzambia huyo.

Hata hivyo Phiri amewataka Simba kama hawamuhitaji waachane naye sasa kwa kumsitishia mkataba wake.

Simba kama itakubaliana na sharti hilo la Phiri watalazimika kutumia mamilioni kumlipa fidia mshambuliaji huyo wa zamani wa Zanaco ya Zambia.