Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pigo Yanga, Pacome kukosekana msimu ujao

Muktasari:

  • Pacome aliumia katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita, Juni 30, 2026 dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Wakati mashabiki wa Yanga wakitambia usajili wa mshambuliaji Peter Shalulile, kuna habari ambayo inaweza kuwapa huzuni juu ya kiungo wao kipenzi, Pacome Zouzoua.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema kwamba mchezaji huyo aliyeumia katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu msimu uliopita dhidi ya JKT Tanzania, hatokuwa sehemu ya kikosi chao msimu ujao.

Kamwe amesema kuwa jina la Pacome limeondolewa katika orodha ya usajili wao msimu ujao ili kumpa nafasi ya kupona akiuguza jeraha lake la mguu uliovunjika.

“Pacome ni mchezaji wetu amesalia na mkataba  kwenye klabu yetu ya Yanga lakini kwa ushauri ambao tumeupata na madaktari, Pacome hatutakuwa naye msimu ujao.

“Kwa hiyo klabu itachukua jukumu lote la kumhudumia kama ambavyo tumefanya kwa wachezaji wengi huko nyuma. Tutamhudumia, ataendelea kuwa kwenye klabu yetu na atapata haki zake zote ambazo anapata kama mchezaji.

“Lakini tumemuondoa kwenye dirisha letu la usajili. Yaani wachezaji ambao tumewasajili kwa ajili ya msimu ujao, Profesa (Pacome), tumemuondoa tunataka apone vizuri. Akishaimarika atarudi msimu ujao kuja kuipambania Yanga yetu. Kwa hiyo habari ni kwamba Pacome Zouzoua hatutakuwa naye msimu ujao,” amesema Kamwe.

Pacome aliumia katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita, Juni 30, 2026 dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na Prince Dube, Maxi Nzengeli na Depu.

Na katika hatua nyingine, Yanga imetangaza kuwa beki wake wa kati na nahodha, Bakari Mwamnyeto, ameongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.