Potter aacha rekodi mbaya zaidi Chelsea
London, England. Graham Potter ameondoka Chelsea akiwa na rekodi mbaya zaidi ya makocha wote waliopita katika kikosi hicho katika histyoria ya klabu hiyo ya Ligi Kuu England.
Potter amekaa na Chelsea kwa takribani miezi sita akichukua nafasi ya mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Thomas Tuchel, Septemba mwaka jana.
Lakini baada ya kuwa na mwenendo mbaya, mmiliki wa Blues, Todd Boehly ameamua kumwondoa kocha huyo wa zamani wa Brighton, akiiacha Chelsea katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
Potter ameondoka akiwa ameshinda michezo sita pekee kati ya 22 ya Ligi Kuu aliyoiongoza miamba hiyo, ikiwa ni kipindi sawa na wakati alipopoteza michezo nane.
Kipigo chake cha mwisho kilikuwa dhidi ya Aston Villa, wajati Chelsea ikizamishwa nyumbani kwa mabao 2-0 na kumkatia tiketi ya kuondoka Stamford Bridge.
Wakati akiwa na wastani wa 1.27 wa pointi kwa kila mchezo, ni Glenn Hoddle ndiye pekee kocha wa zamani wa Chelsea aliyekuwa na kiwango kibaya dhidi ya Potter.
Hoddle alishinda michezo 38 kati ya 122 aliyoiongoza Chelsea, akifungwa mechi 43 na kupata sare 41.
Tuchel, ambaye alitimuliwa miezi minne baada ya Boehly kuinunua klabu hiyo kutoka kwa Roman Abramovich, alikuwa na wastani wa pointi 1.94 kwa kila mchezo (PPG).
Katika kipindi hicho, Tuchel alifanikiwa kucheza mechi 63 za Ligi Kuu England, akishinda 35, sare 17 na kufungwa 11.
Lakini Frank Lampard hadi alipofika Januari 2021, niezi mitano baada ya Tuchel kuichukua tu timu alinyanyua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lampard alikuwa na kiwango kibovu zaidi ya Tuchel, wakati alipoiongoza Chelsea kwenye michezo 57 ya Ligi Kuu England.
Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea, Lampard alishinda michezo 28, akipata sare mara 11 na kupoteza mechi 18, kitu ambacho kilimfanya kutimuliwa baada ya kuinoa timu hiyo kwa miezi 18.
Kwa mshangao, Avram Grant ndiye kocha aliyetimuliwa na Chelsea kati yao akiwa na wastani mzuri wa pointi kwa mchezo (PPG), wakati alipochukua mikoba ya Jose Mourinho, 2007.
Alikaa na kukiongoza kikosi hicho katika michezo 32 pekee, akishinda mechi 22, sare nane na kufungwa mara mbili tu, akifikisha timu kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huo.
Mourinho ianashika nafasi ya pili nyuma ya Grant, alipoichukua timu hiyo na kuiongoza katika michezo 212 ya Ligi Kuu kwenye vipindi viwili, akishinda mechi 140, sare 44 na kufungwa mara 28.
Chelsea sasa inajiandaa kumwajiri kocha wa 19 tangu kuitwa kwa Ligi Kuu England, huku Julian Nagelsmann akionekana kupewa nafasi kubwa ya kumrithi Potter.
Lakini kocha wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino pia anatajwa kuwamo katika orodha, wakati Bruno Saltor akipewa majukumu ya kuwa kocha wa muda.
Potter hakuwa na maneno mengi baada ya mchezo dhidi ya Villa, kama aliyejua kuwa hana muda tena.