Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG yafanya kufuru usajili wa Messi

PSG yafanya kufuru usajili wa Messi

Muktasari:

  • Klabu ya Paris Saint Germain, imekamilisha usajili wa aliyekuwa nahodha na mfungaji bora wa muda wote wa FC Barcelona, Muajentina, Lionel Messi, ambaye alimaliza mkataba wake Juni, mwaka huu ndani ya timu hiyo.

Klabu ya Paris Saint Germain, imekamilisha usajili wa aliyekuwa nahodha na mfungaji bora wa muda wote wa FC Barcelona, Muajentina, Lionel Messi, ambaye alimaliza mkataba wake Juni, mwaka huu ndani ya timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa, Messi, alikuwa amekubali kusaini dili jipya la kuendelea kuitumika Barcelona, lakini dili hilo lilishindwa kukamilika kutokana na sheria ya matumizi ya fedha ambayo iliwataka Barcelona kupunguza mishahara au kuuza baadhi ya mastaa wake kwa ajili ya kuweza kumsajili Messi.

Baada ya dili hilo kushindwa kukamilika, tayari PSG imekamilisha usajili wa nyota huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo, huku kukiwa na kipengele cha kuweza kuongeza mwaka mmoja baada ya mkataba wa awali kumalizika.

Dili hilo lina thamani ya pauni milioni 35 kwa mwaka, litamfanya Messi alipwe mshahara wa pauni milioni moja kwa wiki, ingawa kutokana na makato itamlazimu Messi kupokea pauni 625,000, kwa wiki.

 Agosti 10, mwaka huu, PSG ilimtambulisha nyota huyo na leo atakuwa kwenye dimba la Parc des Princes kwa ajili ya kutambulishwa kwa mashabiki wa timu hiyo ambayo maskani yake ni jijini Paris.