Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afrika ilivyojibu kwa hekima chuki za Gattuso

Muktasari:

  • Timu tisa za Afrika zilizoingia hatua ya 32 bora ni Ivory Coast, Senegal, Misri, Morocco, Cape Verde, DR Congo, Afrika Kusini, Algeria na Ghana huku Tunisia ikiishia makundi.

Baada ya Italia kuwa katika uwezekano finyu wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, mwezi Novemba mwaka jana, kiungo wa zamani wa Italia, Gennaro Gattuso alitoa maoni yaliyotafsiriwa na wengi kuwa ni chuki kwa Bara la Afrika.

Gattuso alionesha kushangazwa na uamuzi wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuamua kulipa Bara la Afrika, nafasi tisa za kufuzu moja kwa moja katika Kombe la Dunia na nafasi moja ya ziada ya kufuzu kupitia mechi za mchujo.

Gattuso alisema kuwa kitendo cha Afrika kuongezewa idadi ya timu, kulileta ugumu katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Bara la Ulaya.

"Enzi zangu, timu zilizomaliza katika nafasi ya pili zikiwa na matokeo bora (katika mechi za kufuzu Ulaya), zilifuzu moja kwa moja. Mwaka 1990 na 1994 kulikuwa na timu mbili tu za Afrika. Sasa hivi kuna tisa. Sio utata lakini inatengeneza ugumu," alisema Gattuso.

Wakati Gattuso akiyasema hayo, alisahau kwamba Bara lake la Ulaya lilikuwa na uwezekano wa kuingiza timu 16 katika fainali hizo lakini hakuamua kuligusa.

Unaweza kutafsiri haraka haraka kwamba ni roho ya ubinafsi na chuki ya Gattuso ndio ilimuongoza kutoa mtazamo huo.

Kwake yeye aliona timu 10 za Afrika ni nyingi kuliko 16 zinazoingia Kombe la Dunia kupitia bara la Ulaya. Ubinafsi ulioje.

Hata hivyo, miezi saba baada ya Gattuso kutoa kauli ile, leo Afrika imemjibu kwa hekima kwa kufanya vizuri ndani ya uwanja.

Timu tisa kati ya 10 kutoka Afrika zimefanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano ya 32 bora ya mashindano hayo.

Timu hizo ni Ivory Coast, Senegal, Misri, Morocco, Cape Verde, DR Congo, Afrika Kusini, Algeria na Ghana.

Hiyo ni sawa na asilimia 90 ya timu zote za Afrika zilizoshiriki huku bara lake la Ulaya likiingiza timu 13 kati ya 16, sawa na asilimia 81.25.

Kufuzu kwa timu hizo tisa za Afrika kwenda hatua ya 32 bora, ni jibu la mwenye hekima kwa mwenye chuki. Mwenye hekima huwa hapayuki bali anatenda.


Mechi za hatua ya 32 bora

Afrika Kusini vs Canada

Brazil vs Japan

Ujerumani vs Paraguay

Uholanzi vs Morocco

Ivory Coast vs Norway

Ufaransa vs Sweden

Mexico vs Ecuador

England vs DR Congo

Ubelgiji vs Senegal

Marekani vs Bosnia&Herzegovina

Hispania vs Austria

Ureno vs Croatia

Australia vs Misri

Argentina vs Cape Verde

Colombia vs Ghana