Ghana yafuata nyayo za Ivory Coast ikiichapa Panama
Muktasari:
- Ghana inakuwa timu ya pili Afrika kupata ushindi katika mechi za kwanza za hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 2026 baada ya Ivory Coast iliyoichapa Ecuador kwa bao 1-1.
Ghana imeanza vyema fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Panama katika mechi iliyochezwa kuanzia saa 8:00 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki, kwenye Uwanja wa Toronto.
Bao pekee la ushindi la Ghana katika mchezo huo limefungwa katika dakika za majeruhi na Yirenkyi Caleb. Caleb amefunga bao hilo akimalizia pasi fupi ya Brandon Asante-Thomas.
Bao hilo la Caleb anayechezea Nordsjaelland inayoshiriki Ligi Kuu Denmark, limeifanya Ghana kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi L linaloongozwa na England, kila moja ikiwa na pointi tatu.
Hata hivyo England ni kinara kwa vile ina utofauti mzuri wa mabao ya kufunga na kufunga kulinganisha na Ghana ambapo yenyewe imefunga manne na kuruhusu mawili.
Lakini pia hii ni mara ya pili mfululizo kwa Caleb kuifungia Ghana kwani alifanya hivyo pia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Wales uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, Juni 2, 2026.
Ghana inakuwa timu ya pili Afrika kupata ushindi katika mechi za kwanza za hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 2026 baada ya Ivory Coast iliyoichapa Ecuador kwa bao 1-1.
Mshambuliaji wa Ghana wakati akijaribu kumtoka beki wa Panama katika mechi ya Fainali za Kombe la Dunia 2026. Picha na Mtandao
Timu nyingine nne zimetoka sare na nne zimeanza kwa kupoteza mechi zao.
Cape Verde imelazimisha sare tasa na Hispania, Misri imetoka sare ya bao 1-1 na Ubelgiji, Morocco ilipata matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Brazil na DR Congo ikatoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ureno.
Afrika Kusini ilianza kwa kuchapwa mabao 2-0 na Mexico, Tunisia ikapigwa mabao 5-1 na Sweden na Senegal ikachapwa mabao 3-1 na Ufaransa.