Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pyramids yagomea ofa ya mayele kwenda Saudi Arabia

Muktasari:

  • Mayele ana nia ya kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia ili kupata changamoto mpya kwenye ligi hiyo inayozidi kuwa maarufu duniani

Cairo, Misri. Klabu ya Pyramids imeripotiwa kukataa ofa ya hivi karibuni kutoka katika klabu ya Al Fateh ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia kwa ajili ya mshambuliaji wao tegemeo, Fiston Mayele.

Mayele, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amekuwa kwenye kiwango bora tangu ajiunge na timu hiyo ya jiji la Cairo, akifunga mabao 39 na kutoa pasi saba za mabao katika mechi 81 alizocheza.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, aliyezaliwa Kinshasa, alikuwa tayari akihusishwa na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, lakini kwa sasa inaelezwa kuwa klabu ya Al Fateh ya Saudi Arabia imeongeza kasi ya kumwania kwa nguvu.

Kwa mujibu wa gazeti la Asharq Al-Awsat la Saudi Arabia limethibitisha kwamba, Al Fateh inamtaja Mayele kuwa chaguo lao kuu kutokana na uwezo wake wa kufumania nyavu na mchango wake mkubwa katika mafanikio ya hivi karibuni ya Pyramids, ikiwemo kutwaa Kombe la Misri msimu wa 2023/24 taji lao kubwa la kwanza kihistoria na ubingwa wa CAF Champions League.

Ingawa thamani ya ofa hiyo haijawekwa wazi, ripoti zinasema kuwa Pyramids FC wameikataa ofa hiyo ya hivi karibuni kutoka Saudi Arabia.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa Mayele ana nia ya kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia ili kupata changamoto mpya kwenye ligi hiyo inayozidi kuwa maarufu kutokana na usajili wa nyota wakubwa duniani.

Mayele, ambaye aliwahi kung’ara pia akiwa na Yanga SC ya Tanzania kabla ya kuhamia Misri, anabaki kuwa mmoja wa washambuliaji wa kuvutia zaidi barani Afrika kwa sasa.