Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Refa alivyotaka kuacha kazi kisa kushambuliwa na mashabiki

Muktasari:

  • Taylor bado ni mwamuzi anayeaminiwa katika Ligi Kuu England na mechi za Ulaya, lakini tukio la Budapest limeacha alama kubwa katika maisha yake binafsi na ya kifamilia.

London, England. Mwamuzi maarufu wa Ligi Kuu England, Anthony Taylor, amefichua kuwa aliwahi kufikiria kuachana kabisa na kazi ya uamuzi baada ya yeye na familia yake kushambuliwa na mashabiki waliokuwa na hasira, kufuatia tukio la fainali ya Europa League mwaka 2023.

Tukio hilo lilitokea mjini Budapest, Hungary, muda mfupi baada ya mchezo kati ya Sevilla na AS Roma, uliomalizika kwa mikwaju ya penalti na Sevilla kutwaa ubingwa.

Kocha wa Roma, José Mourinho, alikasirishwa na maamuzi ya Taylor na baadaye kumkabili nje ya uwanja huku akimtukana kwa maneno makali.

“Bila shaka, hilo ndilo tukio baya zaidi niliwahi kupitia katika maisha yangu ya uamuzi. Sio tu kwa sababu nilikuwa na familia yangu, bali pia lilionyesha namna tabia za watu zinavyoweza kuwa na athari kubwa kwa wengine,” Taylor aliambia BBC Sport

Baada ya mechi hiyo, Taylor na familia yake walivamiwa na zaidi ya mashabiki 100 wa Roma katika Uwanja wa Ndege wa Budapest, waliokuwa wakitupa vitu na kutoa matusi makali.

Walilazimika kujificha katika chumba cha nyuma huku walinzi wakihangaika kuzuia umati huo wenye hasira.

Taylor alisema kuwa tukio hilo lilimfanya ajitafakari kama kweli kazi ya uamuzi anafaa kuendelea nayo.

“Kuna nyakati nyingi nimejiuliza, ‘inafaa kweli kuendelea?’ Kwa sababu unajikuta unalaumiwa kwa mambo ambayo wakati mwingine si kosa lako.”

Alisema tatizo la mashambulizi ya maneno dhidi ya waamuzi ni kubwa sana kwenye soka, kuanzia viwango vya juu hadi vya chini.

“Kuna huu mtazamo wa kizamani kwamba ili kushinda, lazima umshambulie mwamuzi au waamuzi wa pembeni. Hii tabia imekuwa sehemu ya utamaduni wa soka, na ni mbaya,” amesema Taylor.

Katika mchezo huo, Mourinho alimshutumu Taylor kwa “kuwa kama Mhispania” kutokana na idadi ya kadi za njano alizotoa kwa wachezaji wa Roma, na baadaye akamfuata hadi eneo la maegesho ya magari akimtukana kwa maneno ya matusi kwa Kiingereza na Kiitaliano.

Taylor, mwenye umri wa miaka 46, amesema anatarajia kuona mabadiliko makubwa katika namna mchezo unavyolindwa na vyombo vya soka.

“Ikiwa tunataka soka liwe mazingira bora kwa wote, lazima tuanze kupinga utamaduni huu wa matusi na chuki, kuanzia ngazi ya juu hadi mashindanoni mtaani,” amesisitiza.

Taylor bado ni mwamuzi anayeaminiwa katika Ligi Kuu England na mechi za Ulaya, lakini anasema tukio la Budapest limeacha alama kubwa katika maisha yake binafsi na ya kifamilia.