Kocha Liverpool amfuta kazi mwamuzi England
Muktasari:
- Coote alisimamishwa kazi Novemba 11 kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikidaiwa kumuonyesha akitoa matamshi ya dharau dhidi ya Liverpool na kocha wake wa zamani Jürgen Klopp.
London, England. Mwamuzi wa Ligi Kuu ya England, David Coote (42), amefutwa kazi rasmi na shirika la waamuzi wa soka, PGMOL (Professional Game Match Officials Limited), baada ya uchunguzi wa kina kuhusu mwenendo wake wa hivi karibuni.
Coote alisimamishwa kazi Novemba 11, kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikidaiwa kumuonyesha akitoa matamshi ya dharau dhidi ya Liverpool na kocha wake wa zamani Jürgen Klopp, video hiyo ilisababisha mjadala mkubwa huku baadhi ya mashabiki na wachambuzi wa mchezo huo wakionyesha kutoridhishwa na tabia ya mwamuzi huyo.
Tuhuma dhidi ya refa huyu ziliongezeka baada ya gazeti la The Sun kuchapisha picha zinazodaiwa kumuonyesha akitumia dawa za kulevya aina ya cocaine, hatua iliyosababisha afanyiwe uchunguzi zaidi na shirika la waamuzi PGMOL.
David Coote, amechezesha michezo 493 katika mashindano yote huku akifanya hivyo mara 112 kwenye Ligi Kuu England, kwenye ligi daraja la kwanza England amechezesha michezo 143 huku akiwa ametoa kadi za njano 1,762 wakati kadi nyekundu ametoa 117 katika mashindano yote aliyochezesha.
Mwamuzi huyo alianza kuchezesha mchezo wake wa kwanza Aprili 2018 kwenye mchezo kati ya West Brom ambayo ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle wakati mchezo wa mwisho alichezesha mechi kati ya Liverpool iliyopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Aston Villa Novemba 9, 2024.
Michezo aliyochezesha hivi karibuni:
Nov 9, 2024 Liverpool 2-0 Aston Villa
Oct 27, 2024 West Ham 2-1 Man Utd
Oct 6, 2024 Brighton 3-2 Spurs
Sep 21, 2024 Crystal Palace 0-0 Man Utd
Aug 31, 2024 Leicester 1-2 Aston Villa
Aug 25, 2024 Bournemouth 1-1 Newcastle
Aug 16, 2024 Coventry 3-2 Oxford Utd
Aug 13, 2024 Grimsby Town 1-1 Bradford
May 4, 2024 Arsenal 3-0 Bournemouth
Apr 27, 2024 Wolves 2-1 Luton
Apr 14, 2024 Arsenal 0-2 Aston Villa
Mar 31, 2024 Liverpool 2-1 Brighton
Mar 3, 2024 Burnley 0-2 Bournemouth
Feb 28, 2024 Chelsea 3-2 Leeds
Feb 18, 2024 Luton 1-2 Man Utd
Feb 10, 2024 Ipswich 2-2 West Brom
Jan 31, 2024 Spurs 3-2 Brentford
Jan 28, 2024 Newport 2-4 Man Utd
Jan 14, 2024 Everton 0-0 Aston Villa
Jan 10, 2024 Liverpool 2-1Fulham