Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo alipua CAF sakata la AFCON 2025

Nyota wa soka duniani na mshambuliaji wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo

Muktasari:

  • Kupitia ujumbe wake uliosambaa kwa kasi mitandaoni, Ronaldo amesisitiza kuwa haki haikutendeka, akisema matokeo ya uwanjani yanapaswa kuheshimiwa.

Dar es Salaam. Sakata la kutatanisha kuhusu ubingwa wa AFCON 2025 limechukua sura mpya baada ya nyota wa soka duniani Cristiano Ronaldo kuibuka hadharani na kulaani vikali uamuzi wa CAF kuivua Senegal ubingwa na kuivisha Morocco.

Kupitia ujumbe wake uliosambaa kwa kasi mitandaoni, Ronaldo amesisitiza kuwa haki haikutendeka, akisema matokeo ya uwanjani yanapaswa kuheshimiwa.

Kauli hiyo imeongeza shinikizo kwa CAF, huku mijadala mikali ikiendelea miongoni mwa mashabiki, wachambuzi na viongozi wa soka barani Afrika.


Mgawanyiko mkubwa wa maoni

Kauli ya Ronaldo imepokelewa kwa hisia tofauti.

Wapo wanaomuunga mkono wakidai Senegal wameonewa, huku wengine wakitaka ushahidi kamili na ufafanuzi rasmi kutoka CAF kuhusu sababu za mabadiliko hayo ya matokeo.

Wakati huo huo, mchambuzi wa soka wa Uingereza Jamie Carragher ameibua mjadala mwingine kwa kudai kuwa tukio hilo linaonyesha udhaifu wa AFCON, akisema hali kama hiyo haiwezi kutokea katika mashindano ya Ulaya.

 Kauli yake imekosolewa vikali na wadau wengi wa soka Afrika.


Vitisho vya adhabu nzito

Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa iwapo Senegal watakataa kurejesha kombe, medali na zawadi za fedha, wanaweza kukumbana na vikwazo vizito, ikiwa ni pamoja na kufungiwa kushiriki mashindano ya CAF katika ngazi zote, kuzuiwa kushiriki michuano ya kufuzu Kombe la Dunia, klabu zao kutoshiriki mashindano ya kimataifa na wachezaji kunyimwa tuzo na heshima za bara.

Hatua kama hizi, iwapo zitatekelezwa, zinaweza kuwa na athari kubwa kwa maendeleo ya soka nchini Senegal.


Mvutano ndani ya CAF

Ndani ya CAF, taarifa zinaonyesha kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa.

Baadhi ya marais wa vyama vya soka barani humo wanadaiwa kuwa na wasiwasi juu ya ushawishi wa makamu wa rais wa CAF, Faouzi Lekjaa.

Aidha, inadaiwa kuwa Samuel Eto'o aliwasilisha malalamiko rasmi kwa rais wa CAF Patrice Motsepe, akieleza kutoridhishwa na namna maamuzi yanavyofanyika.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Michezo wa Afrika Kusini Gayton McKenzie ameahidi kuisaidia Senegal katika mapambano yao ya kutafuta haki.


Mustakabali wa soka la Afrika hatarini

Wachambuzi wanaonya kuwa sakata hili linaweza kuathiri taswira ya soka la Afrika kimataifa ikiwa CAF haitatoa ufafanuzi wa wazi na wa kuridhisha.

Baadhi wanahofia kuwa hali hiyo inaweza kuchochea mgawanyiko mkubwa au hata wito wa kususia mashindano ya CAF.