Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RT yampigia chapuo Simbu

Historia imeandikwa kwenye mashindano ya Dunia ya Riadha 2025 baada ya mwanariadha, Alphonce Simbu kuibuka kinara wa mbio hizo na kuipa Tanzania medali ya dhahabu ya kwanza kwenye mashindano hayo yaliyofanyika asubuhi ya leo Septemba 15, 2025 Jijini Tokyo, Japan.

Simbu ameandika historia hiyo baada ya kumaliza mbio za kilomita 42 kwa saa 2:09.48 huku akipata upinzani mkali kutoka kwa Amanal Petros wa Ujerumani ambaye pia alikimbia muda sawa (2:09.48) na kushika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Iliass Aouani wa Italia.


Muktasari:

  • ” Simbu ameweka rekodi ya kipekee kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufuzu katika hatua ya mwisho ya tuzo za mwanariadha bora wa dunia katika kipengele cha mbio za nje ya uwanja, zinazotelewa na Shirikisho la Ridha Duniani (WA)”.

Arusha. Zikiwa zimesalia siku mbili pekee kufungwa kwa zoezi la upigaji kura za kuwatafuta wanariadha bora duniani kwa mwaka 2025, Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limewaomba wadau kumpigia kura nyota wa mbio ndefu, Alphonce Simbu, ili kuweka historia mpya kwa taifa.

Simbu ameweka rekodi ya kipekee kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufuzu katika hatua ya mwisho ya tuzo za mwanariadha bora wa dunia katika kipengele cha mbio za nje ya uwanja, zinazotolewa na Shirikisho la Ridha Duniani (WA).

Safari yake imefika hatua ya fainali akichuana na Mkenya, Sebastian Sawe, mshindi wa mbio maarufu za London marathon na Berlin marathon.

Kwa upande wa Simbu, umahiri wake ulionekana wazi baada ya kuibuka mshindi katika marathoni za dunia iliyofanyika Septemba mwaka huu, Tokyo, Japan, hatua iliyompa nafasi ya kuingia kwenye orodha ya majina makubwa duniani.

Rais wa RT, Rogath John Stephen Akhwari, amesema ni muda wa Watanzania kusimama pamoja kumlinda na kumuinua shujaa wao, akisisitiza kuwa kura za Watanzania zina uzito mkubwa wa kumfanya nyota huyo kushinda.

“Hii ni nafasi adhimu kwa taifa, Simbu sio tu ameiwakilisha Tanzania, bali ameipeleka kwenye ramani ya dunia, tunaomba Watanzania wote ndani na nje ya nchi kumpigia kura, tunaamini kabisa Simbu ana uwezo na nafasi ya kushinda”, amesema Akhwari.

Zoezi la kupiga kura kwa nyota waliotinga fainali lilianza Novemba 4 mwaka huu kupitia tovuti ya shirikisho la riadha la dunia na linatazamiwa kukamilika Novemba 9, ambapo washindi watatangazwa kwenye usiku wa tuzo ambazo zitafanyika Novemba 30 jijini Monaco, Ufaransa.

Katika makundi mengine ya tuzo hizo, wapo wanariadha waliopenya kama vile bingwa wa dunia kuruka vihunzi mita 400, Femike Bol wa Uholanzi na bingwa wa dunia mita 400, Sydney McLaughlin-Levrone wa Marekani wanaowania tuzo za mwanariadha bora wa mbio za uwanjani wanawake.

Wengine ni mshindi wa dunia mita 200, Noah Lyles (Marekani), Emannuel Wanyonyi (Kenya), mshindi wa dunia mita 800, upande wa wanaume.

Wapo pia bingwa wa dunia kuruka mbali, Tara Davis- Woodhal (Marekani), bingwa wa dunia kuruka juu, Nicola Olyslagers (Australia) katika tuzo za mwanariadha bora wa fani za uwanjani wanawake, bingwa wa dunia kuruka kijiti, Mondo Duplantis (Sweden) na bingwa wa dunia kuruka mbali, Mattia Furlani wa Italia, upande wa wanaume.

Upande wa mwanariadha bora wa kike wa mbio ndefu nje ya uwanja wapo Peres Jepchirchir kutoka Kenya ambaye ni bingwa wa marathoni wa dunia, pia bingwa wa dunia wa mbio za kutembea, mbio za kilomita 20 na 35, Maria Perez wa Hispania.