Saido, Ambundo watimuliwa kambini Yanga

Wednesday May 25 2022
saido pic
By Mwandishi Wetu

SIKU mbili kabla ya mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Simba na Yanga, kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewatimua Saido Ntibazonkiza na Dickson Ambundo kambini mjini Shinyanga.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba, sababu za kutimuliwa kwao inatajwa kuwa ni kutoroka kambini na kwenda mtaani kinyume na utaratibu.

Simba na Yanga watakwaana Jumamosi Mei 28 katika mchezo ambao utaamua nani atacheza hatua ya fainali na timu hizo zinakutana zikiwa na kumbukumbu ya kugawana pointi kwenye michezo miwili ya ligi msimu huu.


Kupata undani wa taarifa hii pata nakala ya gazeti la Mwanaspoti kesho Mei 26, 2022


Advertisement
Advertisement