Sakata la Fei Toto, Yanga kusikilizwa tena

Muktasari:

  • Kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' alifika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji leo Aprili 12, 2023 kujua hatma ya barua yake ya kuomba kuvunja mkataba na klabu ya Yanga.

Dar es Salaam. Kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' alifika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji leo Aprili 12, 2023 kujua hatma ya barua yake ya kuomba kuvunja mkataba na klabu ya Yanga.

Fei Toto aliongozana na wakili wake Fatma Karume ambaye baada ya kumaliza kusikilizwa leo amesema kuna vitu vya kisheria vinatakiwa kuwasilishwa Aprili 18 na 25 na Mei 4 ndipo rasmi shauri litasikilizwa tena.

"Tunasubiri Mei 4 tutasikilizwa," amezungumza Karume ambaye aliulizwa kuhusu uelekeo wa sakata hilo na kusema hana chochote cha kuzungumza.

Mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick amesema madai yoyote ambayo Fei anayo hata akitaka kuvunja mkataba ofisini kuzungumza.

"Anayemuhitaji Feisal aje klabuni au yeye akitaka kuondoka aje klabuni utaratibu anaujua tupeane mkono wa kwaheri," amesema Patrick