Sarr aipa Simba milioni 50 za Kombe la Muungano

Baada ya kufunga bao pekee katika mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano, kiungo wa Simba Babacar Sarr ameipa timu hiyo kitita cha tsh50 milioni  ambacho ni zawadi ya mshindi wa kwanza wa michuano hiyo.

Sarr alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 77 akiunganisha  mpira wa faulo  ikiwa ni matokeo ya madhambi aliyofanyiwa Willy Onana karibu na wa katikati ya kiwanja.

Mbali ya kupoteza mchezo  Azam  ilionekana kuchangamka zaidi kipindi chapili cha mechi ambapo ilifanya mshambulizi kadhaa lakini hayakuzaa matunda.

Hii inakuwa ni mara ya sita kwa Simba kuchukua ubingwa wa michuano hii ikiwa imeipata Yanga  ambayo pia imechukua mara sita.

Michuano ambayo imefanyika uwanja wa Aman, visiwani Zanzibar  imerejea kwa mara ya kwanza baada ya kusimama kwa takribani miaka 20 ambapo  awali ilikuwa ikishirikisha timu nane,nne kutoka Tanzania Bara na nyingine Zanzibar, lakini sasa limerudi na timu nne tu.

Simba ilifika fainali baada ya kuichapa KVZ mabao 2-0 yaliyofungwa na straia wao Fredy Michael na beki Israel Mwenda, wakati ikifika kwa kuiondosha KMKM kwa kichapo cha mabao 5-2.

Mbali ya zawadi ya mshindi wa kwanza, Azam ambayo imeshiriki michuano hii kwa mara ya kwanza pia ilijizolea tsh30 milioni.

Baada ya mchezo kapteni wa Simba Mohamed Hussen alisema"Nawapongeza Azam wana timu nzuri lakini pia niwapongeze wachezaji wenzangu kwa sababu walipambana vyakutosha. Haikuwa fainali rahisi ndio maana unaona tumepata ushindi wa bao moja"

Kwa upande wa kapteni wa Azam Yahya Zayd aliwapongeza Simba kwa ubingwa na kusema wao wamekubaliana na kile kilichotokea na wanaangalia mbele.