Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yajipanga kuvuna utalii AFCON 2027

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Chande akizungumza bungeni wakati akijibu hoja za wabunge. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Mashindano haya yanatarajiwa kuzikutanisha nchi mbalimbali za Afrika, na kuweka Tanzania katika ramani ya kimataifa kama moja ya vituo muhimu vya michezo na utalii.

Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikijiandaa kuwa mwenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, Serikali imeanza kuweka mikakati mahsusi kuhakikisha sekta ya utalii inanufaika ipasavyo na ujio wa maelfu ya wageni kutoka mataifa mbalimbali.

Akizungumza bungeni leo Aprili 21, 2026, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Chande amesema maandalizi yamefikia hatua nzuri, huku akibainisha kuwa wataalamu wa sekta hiyo tayari wameanza kutoa mafunzo kwa wajasiriamali ili kuwajengea uwezo wa kuhudumia wageni watakaohudhuria mashindano ya AFCON 2027.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wageni hao hawaishii kushuhudia michezo pekee, bali wanapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini, hatua itakayochochea mapato ya sekta hiyo na kukuza uchumi wa wananchi.

“Tumeshajipanga vya kutosha. Wataalamu wetu wanaendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali wetu wadogo na wa kati ili wawe tayari kupokea wageni na kuwapa huduma bora zitakazowavutia kutembelea vivutio vyetu,” amesema Chande.

Kauli hiyo ameitoa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge Lucy Mwakyembe, aliyetaka kufahamu mikakati ya Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo kunufaika na ujio wa wageni hao.

Katika majibu yake, Naibu Waziri amesisitiza kuwa Serikali inaona mashindano hayo kama fursa adhimu ya kuitangaza Tanzania kimataifa, si tu katika michezo bali pia katika utalii, utamaduni na huduma za ukarimu.

Ameongeza kuwa kupitia maandalizi hayo, wajasiriamali watawezeshwa kutumia vyema fursa ya ongezeko la wageni kwa kutoa huduma zenye viwango, jambo litakalosaidia kuongeza muda wa wageni kukaa nchini na kuongeza mapato ya taifa.

Fainali za AFCON zimepangwa kufanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 18 mwakani katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania zikishirikisha timu 28.