Shah Rukh Khan tajiri namba moja duniani
Kwa mujibu wa ripoti ya Hurun India Rich List 2025 imetaja orodha ya wasanii watano wenye utajiri mkubwa zaidi duniani na staa wa India, Shah Rukh Khan akiongoza namba moja kwenye orodha hiyo.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa muigizaji huyo kuingia kwenye listi hiyo na anakadiriwa kuwa na utajiri wa rupia 124.9 bilioni ambazo ni sawa na Shilingi 3.5 trilioni za Tanzania.
Staa huyo wa Bollywood amewazidi mastaa maarufu duniani kama Taylor Swift mwenye utajiri wa dola 1.3 ambazo ni sawa na Shilingi 3.19 trilioni za Tanzania,
Arnold Schwarzenegger (dola bilioni 1.2), Jerry Seinfeld (dola bilioni 1.2) na Selena Gomez (dola milioni 720).
Kwa duniani staa huyo aliyetamba kwa kuigiza kwenye nyimbo kama Kuch Kuch Hota Hai, Koi Mil Gaya, Tujh Mein Rab Dikhta Hai na nyinginezo mara kadhaa alitajwa kwenye tovuti mbalimbali nchini India kuwa nyota mwenye utajiri mkubwa zaidi.
Utajiri wake
Mbali na kumiliki kampuni ya utayarishaji wa filamu ya Red Chillies Entertainment aliyoianzisha mwaka 2002, SRK pia anamiliki hisa kubwa katika timu ya kriketi Knight Riders Sports ambayo ni miongoni mwa timu maarufu na yenye mafanikio kibiashara nchini India.
Inaelezwa pia vyanzo vya utajiri wake vinatokana na nyumba za kifahari alizojenga ikiwemo ile ya Mumbai iliyoko iliyoko Bandra, ikikadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya rupia bilioni 2 ambazo ni zaidi ya Sh60 bilioni za Kitanzania.
Anamiliki mali katika maeneo mengine ya kifahari kama Park Lane (London), Beverly Hills (Marekani) na nyingine zilizopo Dubai.
Mbali na nyumba pia anamiliki magari ya kifahari kama Bugatti Veyron lenye zaidi ya Bilioni 2, Rolls Royce Phantom (Bilioni 2), Bentley Continental GT (Milioni 900) na nyinginezo.
Filamu mpya
Kwa upande wa kazi, SRK yupo kwenye maandalizi ya filamu yake mpya King inayoongozwa na Siddharth Anand. Filamu hiyo inatarajiwa kumshirikisha pia binti yake Suhana Khan na wasanii wengine Abhishek Bachchan, Deepika Padukone, Rani Mukerji na wengineo