Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Azam zavutwa shati Ligi Kuu

Muktasari:

  • Simba imelazimishwa suluhu dhidi ya TRA United wakati Azam nao wakipata matokeo kama hayo dhidi ya Mbeya City .

Matokeo ya 0-0 ambayo Simba imepata Alhamisi dhidi ya TRA United, huku Azam nayo ikibanwa na Mbeya City, kwa kiasi fulani imezidi kuichongea Yanga barabara ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara ambapo sasa ipo kileleni kwa tofauti nane dhidi ya timu ya pili.

Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 44 ikicheza mechi 18, inafuatiwa na Simba yenye 36 kwa mechi 17, kisha Azam inazo 34 ikikamata nafasi ya tatu na mechi zake 18.

Katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Simba ilianza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikijaribu kusaka bao la mapema, lakini TRA United ilionekana kuwa bora kulinda wakiongozwa na nahodha wao, Nassry Kombo huku ikitumia idadi kubwa ya viungo, akiwemo Jamali Dulazi, Chanda Chewe na Ally Ng'anzi kudhibiti presha ya mshambulizi ya wekundu hao wa Msimbazi.

Kocha wa TRA United, Etienne Ndayiragije alionekana kuingia na mpango mzuri ambapo wachezaji wake waliongeza presha ya kutafuta mpira mara tu wanaposogea katika nusu ya pili ya uwanja kwa kutumia muundo ya pembe tatu.

Tofauti na ilivyokuwa katika mechi tano zilizopita za Simba dhidi ya TRA, mechi hii vijana wa Steve Barker walishindwa kupata bao katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, TRA United ilikuwa ikiwasubiri na baada ya kunasa mpira ilitumia kasi ya wachezaji wake wa pembeni akiwemo Ramadhan Chobwedo katika mashambulizi ya kushtukiza.

Simba ilirejea kipindi cha pili na kujaribu kuifungua ngome za TRA huku baada ya dakika 14 za kipindi cha pili ikifanya mabadiliko mawili kwa mpigo, ilimtoa kiungo wa kati, Alassane Kante na winga Libasse Guaye huku wakiingia Clatous Chama na Morice Abraham ili kuongeza nguvu katika eneo la mwisho.

Hata hivyo, TRA United iliendelea kucheza kwa nidhamu ya kujilinda huku katika kipindi hicho cha pili ikionekana kuwa na idadi kubwa zaidi ya wachezaji nyuma tofauti na kipindi cha kwanza ambapo ilikuwa na ukuta wa wachezaji wanne, akiwemo Kombo na Mganda, Christopher Tebandeke ambaye alimpa wakati mgumu, Seleman Mwalimu.

TRA United ilijikuta ikimaliza pungufu katika mchezo huo kufuatia, Nouma kuonyeshwa kadi ya pili ya njano katika dakika ya 88, kadi ya kwanza alionyeshwa katika dakika ya 82.  


AZAM SARE KIBAO

AZAM imeendelea kuangusha pointi kupitia matokeo ya sare baada ya kumaliza dakika 90 zingine bila kufungana ugenini dhidi ya Mbeya City, hii ni sare ya kumi katika Ligi Kuu Bara msimu huu ikiwa ndiyo timu yenye sare nyingi zaidi. Kati ya sare hizo, saba Azam imetoka uwanjani bila kufungana.

Matokeo hayo pale Uwanja wa Tanzanite Kwaraa jijini Babati mkoani Manyara dhidi ya Mbeya City, yanaifanya Azam kufikisha pointi 34 ikisalia nafasi ya tatu.

Kwa upande wa Mbeya City, sare hiyo inazidi kuamsha matumaini ya kujinasua kule chini ikifikisha pointi 17 kunako nafasi ya 12.