Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Singida BS kibaruani leo Kagame Cup

Muktasari:

  • Singida Black Stars ndio bingwa mtetezi wa Kombe la Kagame baada ya kulitwaa mwaka jana huku mara ya mwisho kwa Simba kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ikiwa ni 2002.

Dar es Salaam. Simba na Singida Black Stars leo zinaanza mbio za kuwania taji la Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) 2026 kwa kukabiliana na timu za Jamus na Mogadishu City katika mechi zitakazochezwa jijini Kigali, Rwanda leo.

Mechi hizo zote mbili leo zitachezwa katika Uwanja wa Pele, uliopo Kigali.

Singida Black Stars ndio itatangulia leo kwa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Jamus ya Sudan Kusini ambayo kwa mujibu wa ratiba, itaanza saa 10:00 jioni kwa muda wa Tanzania.

Wawakilishi hao wa Tanzania, wanaingia katika mechi hiyo kibabe kwani ndio mabingwa watetezi wa mashindano hayo baada ya kulitwaa mwaka uliopita.

Baada ya kukosa matoleo manne mfululizo ya mashindano ya Simba inarejea tena na leo itakabiliana na Mogadishu City ya Somalia katika mchezo wake wa kwanza wa mashindano hayo mwaka huu  utakaochezwa kuanzia saa 1:00 usiku kwa muda wa Tanzania.

Pamoja na kutoshiriki mashindano hayo tangu 2018 ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho, Simba inarudi ikiwa bado ni miongoni mwa wababe wa Kombe la Kagame kwa vile ni miongoni mwa timu mbili ambazo ni mabingwa wa kihistoria wa mashindano hayo.

Wawakilishi hao wa Tanzania pamoja na AFC Leopards ya Kenya, kila moja imetwaa ubingwa wa Kombe la Kagame mara sita na hakluna timu nyingine ambayo imeweza kuzifikia.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba mwaka wa mwisho Simba iliposhiriki mashindano hayo, iliishia katika hatua ya fainali ambayo ilifungwa mabao 2-1 katika mechi va fainali.