Simba waitangulia Yanga Lake Tanganyika, wapita milango tofauti

Sunday July 25 2021
simbaa pic
By Ramadhan Elias

KIKOSI cha Simba kimekuwa cha kwanza kuingia uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, kwa ajili ya mchezo wa fainali ya kombe la Azam (ASFC) dhidi ya Yanga.

Simba imefika uwanjani hapo saa  8:24 mchana wakiongozwa na gari la polisi huku wachezaji na baadhi ya viongozi wa timu hiyo wakiwa wamepanda gari aina ya Coasta.

Dakika nne baadae, Yanga nao walitinga uwanjani hapo wakiongozwa na gari la polisi huku wachezaji na viongozi kadhaa wakiwa ndani ya basi moja na Coster.

Timu hizo mbili zimepitia njia tofauti kuingia uwanjani hapo ambapo Yanga wamepita kulia huku Simba wakiingilia kushoto.

Mechi hiyo inatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni ambapo kila timu itakuwa ikipambana kupata ushindi ili kubeba ubingwa wa ASFC

Advertisement