Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga wadondokea humu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB

Muktasari:

  • Yanga ni bingwa wa kihistoria wa Kombe la Shirikisho la CRDB ikiwa imelitwaa mara tano tangu mashindano hayo yaliporudi upya msimu wa 2025/2026.

Dar es Salaam. Droo ya hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB iliyopangwa leo, Ijumaa, Aprili 17, 2026 imeibua mechi kadhaa za kusisimua za timu ambazo zilionyeshana upinzani mkali katika mechi za Ligi Kuu msimu huu.

Katika droo hiyo, Simba imepangwa kukutana na TRA United, Singida Black Stars dhidi ya Coastal Union, JKT Tanzania dhidi ya Yanga na Mashujaa FC dhidi ya Azam FC.

Simba dhidi ya TRA United ni mechi inayokumbushia pambano la mzunguko wa pili wa Ligi Kuu baina ya timu hizo lililochezwa wiki iliyopita ambalo lilimalizika kwa sare tasa.

Mashujaa dhidi ya Azam nazo zilikutana Aprili 19, 2026 katika mechi ya Ligi Kuu ambayo ilimalizika kwa sare tasa.

Hata hivyo Coastal Union na JKT Tanzania zina fursa ya kulipa kisasi cha mechi za Ligi Kuu zilizopoteza dhidi ya Singida Black Stars na Yanga au kuendeleza unyonge.

Katika Ligi Kuu, Coastal Union ilifungwa bao 1-0 na Singida Black Stars na JKT Tanzania ilichapwa mabao 5-0 na Yanga.

Katika nusu fainali, mshindi wa mechi kati ya Simba na TRA United atakutana na mshindi baina ya Singida Black Stars na Coastal Union na timu itakayoshinda kati ya JKT Tanzania na Yanga itakutana na mbabe baina ya Mashujaa FC na Azam FC.