Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yatangulia Fainali FA ikiipiga Coastal nne

Muktasari:

  • Mechi tatu baina ya Simba na Coastal Union msimu huu zimezalisha idadi ya mabao tisa.

Simba imetinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 leo, Jumamosi, Juni 20, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Mabao ya Simba katika mechi hiyo yamewekwa kimiani na Libasse Gueye, Nickson Kibabage, Rushine De Reuck na Clatous Chama.

Gueye ndiye alitangulia kuipatia Simba bao, katika dakika ya 19 baada kumalizia kwa shuti kali, pasi ya Neo Maema, bao ambalo lilidumu hadi muda wa mapumziko ulipowadia.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kuendelea kutawala mchezo na kulishambulia mara kwa mara lango la Coastal Union ambayo ilionekana kukaa nyuma na kujaribu kushambulia kwa kushtukiza mara moja moja.

Dakika 10 tu baada ya kipindi cha pili kuanza, Simba ilijihakikishia ushindi kwa kupata bao la pili kupitia kwa Nickson Kibabage aliyefunga kwa kuunganisha mpira uliombabatiza kipa wa Coastal Union, Wilbol Maseke baada ya shuti la Libasse Gueye.

De Reuck aliipatia Simba bao la tatu katika dakika ya 75 kwa mkwaju wa penalti ambayo iliamriwa na Refa Abel William baada ya Anthony Mligo kuangushwa katika eneo la hatari la Coastal Union na bao la nne lilipachikwa na Chama katika dakika ya 79 akimalizia kwa shuti kali pasi ya Mligo.

Ushindi huo umeifanya Simba pia iendeleze ubabe dhidi ya Coastal Union msimu huu ambapo imeshinda mara zote tatu ambazo timu hizo zimekutana, mbili ikiwa ni katika Ligi Kuu ya NBC.

Timu hiyo sasa inangoja mshindi wa nusu fainali nyingine baina ya Yanga na Aam itakayochezwa kesho ili ikutane naye katika fainali itakayochezwa Julai 4, 2026.

Simba inaingia hatuabya fainali baada ya kukaa miaka mitano bila kugusa hatua hiyo tangu ilipofanya hivyo mwaka 2021.