Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida hawana jezi za akiba

WALIMA alizeti wa mkoani Singida, Singida Big Stars wamekutana na changamoto ya kukosa jezi za akiba kwenye benchi la ufundi, hii ni baada ya mshambuliaji wao Bruno Gomes kuchaniwa jezi na kukosa mbadala ya kuvaa katika tizi.

Iko hivi; baada ya jezi yake kuchanika mchezaji huyo alitoka nje ya uwanja na kumvua mmoja wa wachezaji aliyekuwa benchi na baadaye kubandika karatasi kuzuia jina na namba ya jezi aliyopewa.

Alitumia dakika 10, uwanjani kucheza na jezi ambayo ilikuwa haisomeki jina wala namba hadi waliposaka jezi nyingine iliyobandikwa namba yake.