Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sintofahamu Ali Kamwe azimia kwa Mkapa, apelekwa hospitali

Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe.

Muktasari:

  • Furaha inapozidi inageuka karaha unaweza kusema hivo baada ya Ali Kamwe kuanguka na kupoteza fahamu akishangilia ushindi wa timu yake.

Dar es Salaam. Wakati mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao baada ya kuichapa CR Belouizdad kwa mabao 4-0 hali sio nzuri kwa Ofisa habari wake, Ali Kamwe ambaye ameanguka na kupoteza fahamu baada ya mchezo huo kumalizika.

Kamwe amekumbana na hali hiyo leo Februari 24, 2024 wakati akishangilia ushindi huo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ambapo ameanguka na kupoteza fahamu.

Kamwe amechukuliwa na kutolewa nje vyumba hivyo kisha kupelekwa hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu akiwa ndani ya gari la wagonjwa.

Katibu wa Madaktari wa Tiba za Wanamichezo nchini, Dr Juma Sufian amethibitisha tukio hilo huku akiomba apewe muda kwani yupo kwenye harakati za kumsaidia msemaji huyo.

"Nikweli Kamwe amepatwa na tatizo la kupoteza fahamu tupeni muda tumsaidie kwa haraka ili arejee kwenye afya yake," amesema Sufian ambaye ni daktari wa zamani wa Yanga.