Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Skudu, Aziz Ki vita nzito Yanga

YANGA imeshatimba jijini Tanga tayari kwa mechi za kuwania Ngao ya Jamii, lakini katika kikosi chao kuna vita moja nzito ya mastaa watatu wa timu hiyo akiwamo Mahlatse ‘Skudu’ Makudubela.

Vita hiyo itakuwa mtihani kwa makocha wa timu hiyo wakiongozwa na Miguel Gamondi ambaye atategua kitendawili cha kumtumia yupi kati ya winga Msauzi, yaani Skudu, Stephane Aziz KI na Crispin Ngushi ambaye amerudi na moto kikosini kwa sasa.

Chanzo cha vita hiyo ni Ngushi na tangu atue Gamondi amekuwa kama amezaliwa upya, amekuwa hashikiki mazoezini akiwa na kasi ya kukimbiza, lakini utamu zaidi anafunga pia.

Eneo ambalo limezusha vita hiyo ni winga ya kushoto ambayo Skudu ndiye aliyekuja kuifanyia kazi na sasa amejikuta anakabiliana na wawili hao ambao wamehamishiwa huko na Gamondi.

Takwimu zinaonyesha kwenye mechi nne ambazo Yanga imecheza za kirafiki, Skudu amefunga bao moja alipowatungua Magereza Dar  katika ushindi wa mabao 10-0.

Ngushi hakufunga mechi hiyo, lakini akaja kuweka kambani mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Friends Rangers ambao Yanga ilishinda kwa mabao 6-1.

Aziz KI naye hataki masihara na katika mechi hizo mbili akafunga kila mchezo bao moja na wote watatu wamekuwa wakijaribiwa kwa kupishana winga hiyo ya kushoto.

Aziz KI amerejea na kasi kubwa kuelekea msimu mpya na Gamondi baada ya kumjaribu kucheza kama kiungo mshambuliaji (namba 10), kocha huyo sasa amemrudisha winga ya kushoto na ameonyesha kasi kubwa.

Vita hiyo itaamuliwa na Gamondi katika mechi za Tanga wakati Yanga itakapokuwa inatetea Ngao ya Jamii kwa kuanza kucheza na Azam FC keshokutwa na itajulikana nani ataendelea kuaminiwa na Muargentina huyo kucheza winga hiyo ya kushoto.

Kwa sura nyingine winga ya kulia itabaki kuwa vita ya Kikongomani na Gamondi amekuwa akiwapanga Jesus Moloko na Maxi Nzengeli wakipishana katika michezo ambayo wameshacheza hadi sasa.

Yanga katika mechi nne ilizocheza hadi sasa ikiwamo ile ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, ni mchezo mmoja tu ambao haijafunga bao ilipoumana na JKU ya Zanzibar inayojiandaa na mechi za Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Singida Fountain Gate itakayokuwepo pia Tanga kwenye Ngao ya Jamii.

Mapema kocha wa Yanga, Gamondi alinukuliwa anafurahia namna wachezaji wa timu hiyo kuanzia wale aliowakuta na wapya waliosajili wanavyojituma mazoezi na kuonyesha kiu ya ushindani, kitu anachoamini wakiendelea Yanga itakuwa moto zaidi.

Misimu miwili iliyopita Yanga ilitwaa mataji ya Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho (ASFC) na Ngao ya Jamii na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.