Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

#WC2018: England, Argentina zakumbushia 1998

Muktasari:

  • Owen na kocha wake Glenn Hoddle wanakumbuka vyema fainali zilizopigwa Ufaransa mwaka 1998.

London, England. Miaka 20 iliyopita, mshambuliaji kinda, Michael Owen wa England aliweka rekodi ya aina yake katika fainali za Kombe la Dunia.

Owen na kocha wake Glenn Hoddle wanakumbuka vyema fainali zilizopigwa Ufaransa mwaka 1998.

Ni fainali ambazo Hoddle alisema zilikuwa na mvuto ambapo kikosi cha England kilichoshiriki fainali hizo kitabaki katika kumbukumbu yake.

Hoddle alisema mchezo pekee ambao utabaki katika fikra zake ni England dhidi ya Argentina.

Owen akiwa kinda wa miaka 18, alifunga bao, lakini England ilicheza pungufu baada ya nahodha David Beckham kulimwa kadi nyekundu.

Beckham alitolewa kwa kosa la kumfanyia madhambi Diego Simeone katika mchezo huo ambao timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 kabla ya kupigiana penalti.

Pia libero wa England Sol Campbell alifanya kosa kwa ‘kuruhusu’ bao katika mchezo huo.

Paul Ince akiwa kwenye ubora wake, alikosa mkwaju wa penalti sanjari na Nicky Butty.

“Sikuamini tulivyocheza kwa kiwango bora. Kucheza pungufu dakika 73 ilikuwa kazi kubwa na Michael alipofunga nilishangilia ingawa matokeo yalihuzunisha,”alisema Hoddle.