Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs yaichapa Liverpool nusu fainali ya kwanza Carabao

London, England. Tottenham imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool katika nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Carabao iliyochezwa Uwanja wa Tottenham Hotspur usiku wa kuamkia leo Januari 9, 2025.

Lucas Bergvall ndiye aliyefunga bao hilo na kuipa Spurs faida kabla ya mechi ya marudiano itakayofanyika Anfield, Februari 6, 2025.

Liverpool ilionekana kushangazwa na namna ambavyo mfungaji wa bao hilo mwenye umri wa miaka 18 kuendelea kuwepo uwanjani kabla ya kufunga kwani alimchezea faulo beki wa Liverpool, Kostas Tsimikas iliyostahili kadi ya njano ambayo ingeashiria atolewe kwani ingekuwa ya pili.

Tsimikas alikuwa bado hajarudi uwanjani wakati Bergvall akifunga bao hilo, jambo lililozua hasira kutoka kwa kocha mkuu wa Liverpool, Arne Slot.

Kabla ya bao hilo, Dominic Solanke alifunga lakini lilikataliwa na VAR kutokana na kuonekana alikuwa ameotea.

Licha ya kupoteza mchezo huo, lakini Liverpool ilipambana kusaka bao huku beki wake Trent Alexander-Arnold shuti alilopiga likiokolewa na Radu Dragusin karibu na mstari wa goli.

Mapema tu kipindi cha kwanza, Spurs ilimpoteza kiungo wake, Rodrigo Bentancur baada ya kuanguka wakati wa shambulizi la kona, akapatiwa matibabu kwa takribani dakika 10 kabla ya kutolewa uwanjani, nafasi yake ikachukuliwa na Brennan Johnson.

Katika mchezo huo, kocha wa Spurs, Ange Postecoglou, alionyesha imani kwa wachezaji wake vijana akiwatumia Bergvall (18) ambaye ndiye aliyefunga bao hilo, lakini pia kipa mwenye umri wa miaka 21, Antonin Kinsky aliyeonyesha kiwango kikubwa akiwa amejiunga na timu hiyo kipindi hiki cha dirisha dogo akitokea Slavia Prague.

Baada ya kupoteza ugenini, Liverpool wataingia kwenye mechi ya pili ya nusu fainali kuhakikisha inapindua meza na kutinga fainali kwenda kutetea ubingwa huo waliouchukua msimu uliopita kwa kuifunga Chelsea 1-0.

Liverpool ndiyo timu iliyobeba ubingwa wa michuano hiyo mara nyingi (10) ikifuatiwa na Manchester City (8), Manchester United (6), Chelsea na Aston Villa (5).