Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Suti za Azam zazua jambo Yanga

Muktasari:

Katika kile kinachoonekana mashabiki wa Yanga wana kiu ya mafanikio ndani na nje ya uwanja, juzi usiku waliwataka wachezaji wao kuvaa suti pindi wanapokwenda kushiriki mashindano ya kimataifa.

Dar es Salaam. Katika kile kinachoonekana mashabiki wa Yanga wana kiu ya mafanikio ndani na nje ya uwanja, juzi usiku waliwataka wachezaji wao kuvaa suti pindi wanapokwenda kushiriki mashindano ya kimataifa.

Mashabiki hao wa Yanga walitoa kauli hiyo wakati walipojitokeza kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuilaki  timu hiyo kutoka Rwanda ilikocheza mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR na kushinda mabao 2-1.

Baada ya wachezaji kuanza kutoka uwanjani hapo, mashabiki  waliokuwepo walianza kuwapigia makofi na kuwaambia wachezaji hao wanatakiwa wavae suti kama walivyofanya wenzao wa Azam.

Azam ilikuwa ya kwanza kuwasili uwanjani hapo siku hiyo saa 12:15 jioni wakiwa wamevalia suti nadhifu wakitokea Afrika Kusini ilikoichapa Bidvest Wits mabao 3-0 katika mchezo wa raundi ya kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Mashabiki hao walionekana kama hawakupendezwa na timu yao kuvaa filana na sutu fupi za michezo, kabla ya mashabiki hao kuanza kuwatolea maneno kuwa wanatakiwa kubadilika kwani Yanga ni timu kongwe zaidi ya Azam.

“Tunafurahi mmeshinda, lakini basi na nyie muwe mnavaa suti, msafiri ili muonekana kweli ni wa kimataifa, lakini angalia sasa jinsi mlivyovaa kama mmetoka kijiweni,” alisema shabiki mmoja aliyekuwepo uwanjani hapo kuipokea timu hiyo.

“Azam walitua hapa mapema wamependeza na suti zao, tunataka viongozi wa Yanga nao waige mfano huo, timu inapaswa kusafiri wachezaji wakiwa nadhifu, sio kama nyie mlivyorudi hapa mnatuboa mashabiki wenu, sidhani kama Yanga hamna fedha za kununua suti,” alisikika shabiki mwingine.

Jambo hilo lilionekana kuwafurahisha baadhi ya wachezaji wa Yanga walioishia kucheka tu, huku wakiwaahidi mashabiki hao kuwa watalifanyia kazi jambo hilo na kama wakifanikiwa kuvuka raundi hiyo, mchezo ujao watapiga suti kali.

Yanga itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya APR, Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.