Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yapanda viwango Fifa, Argentina bado kinara

Muktasari:

Tanzania imepanda kwa nafasi 13 na kuwa ya 123 katika viwango vya Shirikisho la Soka duniani (Fifa) ambavyo vimetolewa mapema leo.

Tanzania imepanda kwa nafasi 13 na kuwa ya 123 katika viwango vya Shirikisho la Soka duniani (Fifa) ambavyo vimetolewa mapema leo.

Hata hivyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania inatanguliwa na Uganda iliyopo katika nafasi ya 69 kwa ubora wa soka duniani, Kenya (86) baada ya kupanda kwa nafasi 43 na Rwanda katika nafasi ya 111. Burundi ni ya 125.

Hata hivyo, nafasi tano za juu hazijabadilika kwani bado Argentina ipo kileleni mwa msimamo huo, ikifuatiwa na Ubelgiji, Colombia, Ujerumani na Chile.

Msimamo huo wa viwango unazionesha Kenya na New Zealnda zikipanda kwa nafasi 54 juu ambapo New Zealanda imepanda hadi nafasi ya 93 katika ubora wa soka duniani.