Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tiketi Kombe la Dunia 2026 zagombewa kama njugu mtandaoni

Muktasari:

  • Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitafanyika kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, 2026 zikiandaliwa na nchi tatu kwa pamoja ambazo ni Marekani, Canada na Mexico.

Takribani miezi 10 kabla ya kuanza kwa Fainali za Kombe la Dunia 2026 huko Marekani, Canada na Mexico, tiketi kwa ajili ya mashabiki kutazama mechi za fainali hizo zimeanza kugeuka lulu muda mfupi baada ya hatua ya kwanza ya uuzaji wake kuanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ndani ya siku moja baada ya kufunguliwa mchakato wa maombi ya ununuzi wa tiketi kwa njia ya Visa kufunguliwa, zaidi ya watu milioni 1.5 wametuma maombi ya kuhitaji tiketi hizo.

Watu hao waliotuma maombi ya tiketi hizo kupitia njia ya Visa ni kutoka mataifa 210 waliofanya kupitia mtandao wa FIFA.

Taarifa hiyo ya FIFA imeeleza kwamba idadi kubwa ya watu kati ya hao milioni 1.5, inatoka katika nchi za Marekani, Mexico na Canada ambazo zitaandaa fainali hizo kwa pamoja.

Nchi nyingine ambazo mashabiki wake wamechangamkia kwa kiasi kikubwa tiketi hizo ni Argentina, Colombia, Brazil, England, Hispania, Ureno na Ujerumani.

"Idadi kubwa ya maombi yaliyowasilishwa ni uthibitisho wa kiasi kikubwa cha msisimko uliochochewa kote ulimwenguni na Kombe la Dunia la 2026 na kiwango ambacho kiko tayari kuwa kisima katika historia ya kandanda," amesema Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kombe la Dunia 2026, Heimo Schirgi.

Katika Fainali za Kombe la Dunia 2026, idadi ya timu za taifa 48 zitashiriki kutoka mabara tofauti ambazo zitagawanywa katika makundi 12 yenye timu nne kila moja.

Hadi sasa idadi ya timu 18 zimeshafanikiwa kukata tiketi ya kushiriki fainali hizo huku 30 zikisubiriwa kufanya hivyo kupitia mashindano ya kuwania kufuzu yanayoendelea.

Timu 18 ambazo zimefuzu ni Australia, Iran, Japan, Jordan, Korea Kusini, Uzbekistan, Tunisia, Misri, Brazil, Argentina, Colombia, Ecuador, Paraguay, Uruguay, New Zealand, Mexico, Canada na Marekani.

Idadi ya Viwanja 16 vitatumika kwa mechi za mashindano hayo ambapo Vitatu vitakuwa Mexico, kimoja Canada na Marekani itakuwa na viwanja 12.