Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu ya Wanawake ya Iran yazua gumzo

Muktasari:

  • Timu ya taifa ya Wanawake ya Iran inashika nafasi ya 68 katika viwango vya ubora wa Soka kwa wanawake vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA).

Taarifa zimeibuka kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Iran walitoa ishara za kimataifa za kuomba msaada (SOS) walipokuwa wakirejea nyumbani kutoka Australia, baada ya kutajwa kuwa “wasaliti” nchini kwao kwa kukataa kuimba wimbo wa taifa.

Baada ya kumaliza mechi yao ya mwisho ya Kombe la Asia usiku wa Jumapili, Machi 8, 2026, inaripotiwa kuwa mmoja wa wachezaji hao alitoa ishara ya kimataifa ya kuomba msaada kupitia dirisha la basi la timu.

Ishara hiyo hufanywa kwa kuinua kiganja cha mkono kilicho wazi, kuvusha kidole gumba ndani ya kiganja na kisha kukunja vidole vinne juu yake.

Video zilizosambaa mtandaoni zinaonyesha mashabiki, wengi wao wakiwa wamebeba bendera zenye alama ya Simba na Jua, wakikimbia sambamba na basi la timu huku wakipiga kelele wakisema, “waokoe wasichana wetu” na “waacheni waende.”

Tukio hilo limekuja baada ya wachezaji hao kusimama kimya wakati wimbo wa taifa la Iran ulipopigwa kabla ya mechi dhidi ya Korea Kusini Jumatatu. Hatua hiyo ya kupinga ilizua hasira kali kutoka kwa mamlaka za Iran.

Mtangazaji wa televisheni Mohammad Reza Shahbazi, ametoa wito kwa mamlaka kuwatangaza wachezaji hao kuwa wasaliti.

“Naomba niseme jambo moja tu: wasaliti wakati wa vita wanapaswa kushughulikiwa kwa ukali zaidi,” alinukuliwa akisema kulingana na tafsiri ya jukwaa la mitandao ya kijamii la X.

Kauli hizo zinaonekana kuwaathiri wachezaji hao, ambao baadaye walidaiwa kuwa kama “mateka” walipoonekana kuimba wimbo wa taifa kabla ya kupokea kipigo cha mabao 4-0 kutoka Australia siku ya Alhamisi.

Hata hivyo, mashabiki katika mashindano ya Kombe la Asia waliendelea kuwaunga mkono wachezaji hao wa Iran. Wachezaji hao waliimba tena wimbo wa taifa kabla ya kupoteza mechi nyingine kwa mabao 2-0 dhidi ya Ufilipino Jumapili.

Hatua ya awali ya timu hiyo kukataa kuimba wimbo wa taifa ilikuja siku mbili tu baada ya kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, aliyekuwa ametawala nchi hiyo kwa zaidi ya miongo minne kwa mkono mkali.

Akizungumza tena kulaani hatua ya timu hiyo, mtangazaji Shahbazi alisema, “mtu yeyote anayechukua hatua dhidi ya nchi wakati wa hali ya vita lazima achukuliwe hatua kali zaidi. Kama suala hili la timu yetu ya wanawake kutokuimba wimbo wa taifa, na picha iliyochapishwa na mengineyo, ambayo sitaingia kwa undani.”