Unaona chama lako likitoboa kwa ratiba hii EPL?
Muktasari:
- Utepe wa ligi hiyo utakatwa Ijumaa, Agosti 16 ambapo wenyeji Manchester United watawakaribisha Fulham kwenye Dimba la Old Trafford, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa ligi ya msimu wa 2024-25.
London, England. Mapema tu mashabiki wa soka duniani wanaofuatilia Ligi Kuu England 'Premier League' wamepata kufahamu msimu ujao wa 2024-2025 utaanzaje baada ya ratiba ya ligi hiyo kuwekwa hadharani huku mabingwa watetezi Manchester City wakiwa na kibarua cha kuanzia ugenini Stamford Bridge kukabiliana na Chelsea, Agosti 18.
Utepe wa ligi hiyo utakatwa Ijumaa, Agosti 16 ambapo wenyeji Manchester United watawakaribisha Fulham kwenye Dimba la Old Trafford, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa ligi ya msimu wa 2024-25.
Wikiendi ya kwanza tu inaanza kwa moto mkali pale ambapo Kocha Kieran McKenna, akiwa na kibarua cha kuiongoza Chelsea ikiwa nyumbani kukabiliana na mabingwa watetezi Manchester City chini ya bosi wake wa zamani, Pep Guardiola.
Arsenal na kampeni yao ya kujaribu kunasa taji la kwanza la Ligi Kuu England baada ya miaka 20, safari hii itaanzia Emirates ikikipiga dhidi ya Wolves, Jumamosi, Agosti 17.
Mechi nyingine matata kwenye wikiendi ya kwanza, itashuhudia timu iliyopanda daraja, Ipswich Town itakayokuwa nyumbani Portman Road kukipiga na Liverpool, ambayo itakuwa chini ya kocha mpya, Arne Slot baada ya Jurgen Klopp kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita ambaye alidumu na miamba hiyo ya Anfield kwa miaka tisa.
Msimu uliopita Man City ilihitaji ushindi kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya West Ham United na kufanikiwa kuipiku Arsenal kwenye vita ya ubingwa wa ligi hiyo. Kwa upande mwingine wa msimamo, kulikuwa na timu tatu Luton, Burnley na Sheffield United zilishuka daraja na msimu ujao zitacheza Championship.
Kwa maana hiyo, kutakuwa na sura mpya kwenye ligi licha ya kwamba mbili zilishuka daraja mwaka jana, ambazo ni Leicester City na Southampton, zilizorejea kwenye, huku wapya ambao hawakuonekana kwenye Ligi Kuu England kwa zaidi ya miaka 20 ni Ipswich Town.
Msimu wa 2024-25 hakutakuwa na mapumziko ya kupisha kipindi cha baridi kwenye Ligi Kuu England, hivyo wachezaji watapewa muda zaidi wa kumpumzika hasa kwa wale ambao watatoka kwenye fainali za Euro 2024.
Msimu wa 2024-25 utahusisha wikiendi 33 pamoja na mechi za katikati ya wiki kwa wiki nne. Mechi za Boxing Day zitaendelea kuwepo kama ilivyo kwenye utamaduni wa Ligi Kuu England, licha ya msimu mpya hautakuwa na mechi za Mkesha wa Krismasi kama ilivyokuwa kwenye msimu wa 2023-24. Mechi tamu za kipindi cha sikukuu, zinahusisha pia kipute cha London Derby kati ya Chelsea na Fulham, wakati Arsenal yenyewe itakipiga na Ipswich huko Emirates.
Kama ilivyo kawaida, mashabiki wa Ligi Kuu England watapata fursa ya kutazama mechi za mahasimu ambapo kipute cha Merseyside Derby kinachokutanisha Liverpool na Everton kitapigwa Goodison Park, Desemba mwaka huu na marudiano itakuwa Anfield, Aprili mwakani.
Tottenham na Arsenal zitakutana Septemba mwaka huu kwenye mchezo wa kwanza, wakati ule wa marudiano utapigwa Januari huko Emirates, huku Manchester Derby ya kwanza itapigwa Etihad, Desemba na ile ya Old Trafford itapigwa Aprili 2025.
Kwenye wikiendi ya kwanza. Everton, Newcastle United, Nottingham Forest na West Ham zitakipiga na Brighton, Southampton, Bournemouth na Aston Villa. Newcastle, Forest, Southampton, Tottenham na Wolves zitamaliza msimu kwa kucheza na Everton, Chelsea, Arsenal, Brighton na Brentford mtawalia, huku ligi hiyo ikitarajia kushuhudia mechi 380 na tamati yake itakuwa Mei 25, 2025.
MAKOCHA WAPYA WATANO
Ndani ya Premier League ya msimu wa 2024-2025 kutakuwa na makocha watano wakiwa na timu mpya, ikiwa ni pamoja na Arne Slot aliyechukua nafasi ya Jurgen Klopp kwenye kikosi cha Liverpool. Enzo Maresca anaanza maisha yake akiwa Kocha wa Chelsea baada ya kuiongoza Leicester City kurejea Premier, yeye anachukua nafasi ya Mauricio Pochettino. Julen Lopetegui anamrithi David Moyes pale West Ham na kocha mwenye umri wa miaka 31, Fabian Hurzeler, anachukua nafasi ya Roberto De Zerbi kunako kikosi cha Brighton na kuwa kocha mkuu mdogo zaidi katika historia ya Premier League.
MACHO YAPO HAPA
Man Utd vs Fulham
Mechi ya ufunguzi itawakutanisha Man United dhidi ya Fulham ikichezwa Agosti 16 kwenye Uwanja wa Old Trafford, wawili hawa msimu uliopita walipokutana kila mmoja alishinda nyumbani kwa mwenzake. Man Utd msimu wanatarajia kuanza msimu wa 2024/25 vizuri zaidi hivyo katika mechi ya kwanza, tunaweza kushuhudia kitu bora.
Ipswich vs Liverpool
Kurudi kwa Ipswich kwenye Premier League baada ya miaka 22 kupita pamoja na mwanzo wa Arne Slot katika majumu yake ndani ya Liverpool inasubiriwa kwa hamu kubwa siku ya Agosti 17 nini kitatokea.
Everton vs Brighton
Historia itaandikwa Goodison Park wakati kocha mdogo zaidi kuwahi kutokea kwenye Premier League, Fabian Hurzeler mwenye miaka 31 akiiongoza Brighton & Hove Albion, atakapoanza kibarua chake Jumamosi ya Agosti 17.
Chelsea vs Man City
Enzo Maresca ataanzia nyumbani akiwa na chama lake jipya la Chelsea dhidi ya mwalimu wake, Pep Guardiola, kumbuka mchezo huu utakaochezwa Jumapili ya Agosti 18 utakuwa ni mwanzo wa Manchester City kutetea taji lao.
Leicester vs Spurs
Hakuna uhakika bado kuhusu nani atakayekuwa kwenye benchi la Leicester City baada ya kocha aliyewapandisha daraja kuchukuliwa na Chelsea. Mabingwa hawa wa Premier msimu wa 2015-2016, watakuwa nyumbani King Power kuwakabili Spurs. Itakuwa Jumatatu ya Agosti 19.
Aston Villa vs Arsenal
Msimu uliopita Kocha wa Aston Villa, Unai Emery, aliifunga timu yake ya zamani Arsenal nyumbani na ugenini, hivyo huu utakuwa mtihani kwa Arsenal ambayo msimu huu inataka kubeba ubingwa. Mechi yao ya kwanza itachezwa Jumamosi ya Agosti 24.
Man Utd vs Liverpool
Jumamosi ya Agosti 31 tutashuhudia mchezo huu mkubwa ambao utakuwa ni mtihani wa kwanza kwa Kocha wa Liverpool, Slot kuonyesha uwezo wake wa kushinda ndani ya top six.
Spurs vs Arsenal
Mechi nyingine kubwa kwa Arsenal katika mwanzo ambao unaweza kuwa mgumu itakuwa dhidi ya watani zao wa jadi Spurs, itakuwa ni mechi ya nne ya msimu kwa timu hiyo chini ya Mikel Arteta ikiwa ni Dabi ya kwanza ya London Kaskazini ikichezwa Jumamosi ya Septemba 14.
Man City vs Arsenal
Timu mbili bora kutoka misimu miwili iliyopita zitakutana kwa mara ya kwanza msimu huu. Kiungo wa Man City, Rodri, alidai Arsenal walifurahia tu kutoka sare Etihad msimu wa 2023/24. Je, watakuwa na ujasiri zaidi wakati huu? Ngoma itapigwa Jumamosi ya Septemba 21.
Southampton vs Ipswich
Wametoka wote Championship, watakutana tena St Mary's nyumbani kwa Southampton. Itakuwa Septemba 21.
Liverpool vs Chelsea
Mchezo unaokwenda kukutanisha makocha wapya. Slot na Maresca wanakwenda kukutana ikiwa ni nafasi nzuri ya kupima maendeleo yao katika majukumu mapya, hiyo itakuwa Jumamosi ya Oktoba 19.
Leicester vs Chelsea
Maresca aliiongoza Leicester kupanda tena Premier League msimu uliopita, lakini baadaye akavutwa na Chelsea. Anarejea kwenye klabu yake ya zamani akiwa na klabu mpya, mechi ikichezwa Jumamosi ya Novemba 23.
Liverpool vs Man City
Moja ya mechi zenye ushindani mkubwa ndani ya Premier League katika miaka ya hivi karibuni. Je, Slot anaweza kudumisha ushindani uliokuwepo hapo awali kipindi cha Jurgen Klopp na kuhakikisha Liverpool inaendelea kushindana na Man City? Majibu yatapatikana Jumamosi ya Novemba 30.
Arsenal vs Man Utd
Kipigo cha 3-1 ilichopata Man Utd mbele ya Arsenal msimu uliopita kilimchukiza sana kocha Erik ten Hag. Atapata nafasi ya kulipiza kisasi au mambo yatakuwa vilevile? Desemba 3 itaamua.
Everton vs Liverpool
Fursa nyingine kubwa kwa Slot. Siku yake ya kwanza katika Merseyside Dabi akiwa ugenini pale Goodison Park akiwa na Liverpool. Mambo yatakuwa Jumamosi ya Desemba 7.
West Ham vs Wolves
Kurejea kwake viunga vya Molineux itakuwa ni Aprili 2024, lakini kocha mpya wa West Ham, Julen Lopetegui kwanza atakutana na klabu yake ya zamani Desemba 7.
Man City vs Man Utd
Kwa muda mrefu Man City imekuwa ikiitesa Man United ndani ya Premier, lakini tulishuhudia msimu uliopita Man United ikiishangaza Man City katika fainali ya Kombe la FA. Desemba 14 wawili hao watapambana katika Manchester Dabi ya kwanza msimu huu.
Ipswich vs Chelsea
Timu zinazokwenda kukutana hapa moja ni ngeni na nyingine ipo muda mrefu Premier, lakini makocha wanaopambana wote wametokea Championship. Kieran McKenna wa Ipswich anakwenda kukabiliana na Maresca aliyekuwa Leicester. Mechi itachezwa Desemba 29.
Liverpool vs Man Utd
Mechi kubwa inayovutia miongoni mwa mechi za mwanzoni mwa mwaka 2025 ni hii itakayochezwa Jumamosi ya Januari 4 pale ambapo Slot anapowakaribisha Man Utd ndani ya Anfield.
Arsenal vs Spurs
Hapa itakuwa ni wakati ambao Premier inarejea baada ya mapumziko ya mechi za Kombe la FA, itapigwa Dabi ya London Kaskazini Arsenal wakiwa wenyeji wa Spurs, Januari 14, 2025.
Jumamosi 1 Februari - Arsenal vs Man City
Arteta na Guardiola watavunja urafiki wao tena katika kutafuta pointi za Ligi Kuu. Wakitarajiwa kuwa washindani wa ubingwa tena, hii inaweza kuwa tarehe nyingine muhimu katika mbio za kuwa mabingwa.
Man City vs Liverpool
Februari ni mwezi wa kuwa macho zaidi kwa Man City kwani itakabiliwa na mechi ngumu ikiwemo ya nyumbani dhidi ya Liverpool Jumamosi ya Februari 22. Pia watakutana na Arsenal, Newcastle na Spurs, hivyo ni kipindi muhimu kwa mabingwa hao watetezi kuchanga karata zao vyema.
Man Utd vs Arsenal
Arsenal wataelekea Old Trafford Jumamosi ya Machi 8, wakiwa na matumaini ya kurudia ushindi wao wa 1-0 msimu uliopita walipocheza hapo.
Liverpool vs Everton
Aprili 2, 2025 Slot atalazimika kuwakaribisha watani zao wa jadi Everton katika Dabi ya Merseyside pale Anfield ukiwa ni mwezi mmoja kabla ya kufika Mei ya kuhitimisha msimu, hadi wakati huo tunaweza kuipata picha ya wanaowania ubingwa.
Man Utd vs Man City
Licha ya pengo lililokuwa katika ligi kati ya timu hizi mbili, Man City watatakiwa kuwa makini watakapoenda Old Trafford kucheza Manchester Dabi hiyo Aprili 5.
Liverpool vs Arsenal
Mechi ya kuvutia katika hatua muhimu ya msimu - mechi ya tatu kutoka mwisho. Inaweza kuwa ni mechi ngumu hasa kwa upande mmoja au zote kuelekea kuhitimisha msimu. Itachezwa Mei 10, 2025.
Chelsea vs Man Utd
Jumapili ya Mei 18, 2025 itakuwa ni moja kati ya mechi kubwa katika wiki ya mwisho ya msimu, mwezi mgumu kwa Chelsea ambao pia una mechi dhidi ya Liverpool na Newcastle.
RATIBA YA MECHI 10 ZA KWANZA
WIKI YA KWANZA
Man Utd v Fulham
Ipswich Town v Liverpool
Arsenal v Wolves
Everton v Brighton
Newcastle United v Southampton
Nottingham Forest v Bournemouth
West Ham v Aston Villa
Brentford v Crystal Palace
Chelsea v Man City
Leicester City v Spurs
WIKI YA PILI
Bournemouth v Newcastle United
Aston Villa v Arsenal
Brighton v Man Utd
Crystal Palace v West Ham
Fulham v Leicester City
Liverpool v Brentford
Man City v Ipswich Town
Southampton v Nottingham Forest
Spurs v Everton
Wolves v Chelsea
WIKI YA TATU
Arsenal v Brighton
Brentford v Southampton
Chelsea v Crystal Palace
Everton v Bournemouth
Ipswich Town v Fulham
Leicester City v Aston Villa
Man Utd v Liverpool
Newcastle United v Spurs
Nottingham Forest v Wolves
West Ham v Man City
WIKI YA NNE
Bournemouth v Chelsea
Aston Villa v Everton
Brighton v Ipswich Town
Crystal Palace v Leicester City
Fulham v West Ham
Liverpool v Nottingham Forest
Man City v Brentford
Southampton v Man Utd
Spurs v Arsenal
Wolves v Newcastle United
WIKI YA TANO
Aston Villa v Wolves
Brighton v Nottingham Forest
Crystal Palace v Man Utd
Fulham v Newcastle United
Leicester City v Everton
Liverpool v Bournemouth
Man City v Arsenal
Southampton v Ipswich Town
Spurs v Brentford
West Ham v Chelsea
WIKI YA SITA
Bournemouth v Southampton
Arsenal v Leicester City
Brentford v West Ham
Chelsea v Brighton
Everton v Crystal Palace
Ipswich Town v Aston Villa
Man Utd v Spurs
Newcastle United v Man City
Nottingham Forest v Fulham
Wolves v Liverpool
WIKI YA SABA
Arsenal v Southampton
Aston Villa v Man Utd
Brentford v Wolves
Brighton v Spurs
Chelsea v Nottingham Forest
Crystal Palace v Liverpool
Everton v Newcastle United
Leicester City v Bournemouth
Man City v Fulham
West Ham v Ipswich Town
WIKI YA NANE
Bournemouth v Arsenal
Fulham v Aston Villa
Ipswich Town v Everton
Liverpool v Chelsea
Man Utd v Brentford
Newcastle United v Brighton
Nottingham Forest v Crystal Palace
Southampton v Leicester City
Spurs v West Ham
Wolves v Man City
WIKI YA TISA
Arsenal v Liverpool
Aston Villa v Bournemouth
Brentford v Ipswich Town
Brighton v Wolves
Chelsea v Newcastle United
Crystal Palace v Spurs
Everton v Fulham
Leicester City v Nottingham Forest
Man City v Southampton
West Ham v Man Utd
WIKI YA KUMI
Bournemouth v Man City
Fulham v Brentford
Ipswich Town v Leicester City
Liverpool v Brighton
Man Utd v Chelsea
Newcastle United v Arsenal
Nottingham Forest v West Ham
Southampton v Everton
Spurs v Aston Villa
Wolves v Crystal Palace,.