Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uswisi yaishushia kipigo kizito Bosnia Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Mabadiliko matatu ya wachezaji kwa timu zote ambapo Uswizi ikifanya mawili huku Bosnia ikifanya moja, ndio yamekwenda kutengeneza mabao matatu kati ya manne katika mchezo huo.

Uswisi imefanikiwa kuishushia kipigo kizito Bosnia and Herzegovina ikiichapa kwa mabao 4-1, na kwenda kuongoza kundi B katika Fainali za Kombe la Dunia 2026.

Mabadiliko matatu ya wachezaji kwa timu zote ambapo Uswizi ikifanya mawili huku Bosnia ikifanya moja, ndio yamekwenda kutengeneza mabao matatu kati ya manne katika mchezo huo.

Timu hizo zilimaliza dakika 45 za kwanza zikiwa hazijafungana lakini zikitengeneza nafasi nyingi lakini ubora wa makipa wa timu zote zikazifanya kwenda kupumzika bila kufungana.

Kipindi cha pili dakika ya 71 Uswizi iliwaingiza viungo wawili  Johan Manzambi na Ruben Vargas ndio waliokwenda kuubadilisha mchezo huo wakifunga mabao matatu.

Manzambi amefunga mabao mawili dakika za 74 na 90 ambapo moja kati ya hayo akitumia asisti ya Vargas, yakatosha kuipunguza nguvu Bosnia.

Vargas naye akapiga bao lake dakika ya 84 akipokea asisti ya mshambuliaji Breel Embolo na kuihakikishia ushindi timu hiyo.

Wakati Uswizi ikiona imemaliza mechi Bosnia nayo ikapata bao lake dakika ya 90+3 Ermin Mahmic dakika moja tangu aingie uwanjani alimalizia kwa shuti mpira uliopanguliwa na kipa kutokana na shambulizi la kona.

Bao la nne kwa Uswizi likafungwa dakika ya 90+7 na nahodha wa timu hiyo kiungo Granit Xhaka baada ya mwenzake kuangushwa eneo la hatari.

Mapema Bosnia ilipata pigo dakika ya 80 baada ya beki wake Tariq Muharemovic kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Uswizi wakati anakwenda kufunga.