Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utamu EPL uko hapa, Arsenal, Man City kazi wanayo

Muktasari:

  • Man City ndiyo vinara wa ligi Kuu England ikifuatiwa na Brighton huku mabao yakiwatofautisha na Arsenal.

London, England. Ligi Kuu ya England itaendelea tena kesho Agosti 31, 2024 ambapo viwanja saba tofauti vitatimua vumbi, huku mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Arsenal dhidi ya Brighton utakaochezwa saa 8:30 mchana kwenye Uwanja wa Emirates.

Arsenal na Brighton zimekutana mara 14 kwenye mechi za ligi, ambapo Arsenal imeshinda michezo sita, huku Brighton ikishinda mitano na kutoka sare mara tatu.

Mabingwa watetezi wa EPL, Man City itakuwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya West Ham, mchezo utakaopigwa saa 1:30 jioni, huku rekodi zikiibeba City ambapo katika michezo mitano ya mwisho waliyokutana City imeshinda minne huku zikitoka sare mara moja.

Michezo mingine itawakutamisha Brentford dhidi ya Southampton, Everton dhidi ya Bournamouth, Ipswich dhidi ya Fulham, Leicester dhidi ya Aston Villa pamoja na Nothingham Forest dhidi ya Wolves yote itachezwa saa 11:00 jioni.