Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Owen aitabiria Arsenal ubingwa EPL

Muktasari:

  • Michael Owen ametabiri kuwa Arsenal kutwaa ubingwa wa EPL msimu ujao, akionyesha kuwa Man United haitakuwa kwenye nafasi nne za juu.

London. Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Michael Owen ametabiri Arsenal kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) msimu ujao wa 2024/2025 huku akishindwa kuiweka Man United katika orodha ya timu nne zitakazomaliza katioka nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Owen ambaye pia amewahi kuichezea Liverpool, anaamini kuwa Arsenal itazima ubabe wa Man City na kutwaa ubingwa wa EPL baada ya kuukosa msimu uliopita ilipozidiwa kwa pointi mbili mwishoni mwa msimu.

Katika utabiri wake alioutoa katika mtandao wa EPL jana, Owen ameiweka Liverpool kumaliza katika nafasi ya pili, Aston Villa kumaliza katika nafasi ya tatu na Man City kumaliza katika nafasi ya nne.

Utabiri wa Michael Owen kuwa Arsenal itachukua ubingwa wa EPL, umefanana na ule wa nyota wa zamani wa Tottenham Hotspur, Darren Bent ambaye naye anaamini kitu kama hicho.

Hata hivyo Bent ametofautiana na Owen katika nafasi tatu zinazofuata kwenye msimamo ambapo yeye ametabiri nafasi ya pili kuchukuliwa na Man City, Liverpool kuwa nafasi ya tatu na ile ya nne kuchukuliwa na Chelsea.

Hata hivyo kundi kubwa la wachambuzi limeonekana kuitabiria zaidi Man City kutwaa ubingwa huku Arsenal ikitabiriwa kumaliza katika nafasi ya pili.

Kati ya wachambuzi nane waliotoa utabiri wao, sita wametabiri Man City itachukua ubingwa na ni Owen na Bent tu ambao wameenda kinyume nao.

Karen Carney, Tim Sherwood, Mark Schwarzer, Shay Given, Don Hutchison na Matt Holland wote wametabiri kuwa bingwa wa msimu ujao atakuwa ni Man City.

Utabiri wa Carney umetaja Man City kuwa bingwa, Arsenal katika nafasi ya pili, Liverpool ya tatu na nafasi ya nne ni Manchester United wakati Sherwood nne bora yake ina Man City, Arsenal, Man United na Tottenham Hotspur.

Shay Given ameanza na Man City kisha Liverpool, Arsenal namba tatu na ya nne ni Newcastle United huku Mark Schwarzer akizitaja Man City, Arsenal, Liverpool na Spurs mtawalia.

Nne boora ya Don Hutchison ina Man City, Arsenal, Liverpool na Spurs na Matt Holland amezitaja Man City, Arsenal, Liverpool na Man United.

Ligi Kuu England msimu wa 2024/2025 utaanza rasmi Ijumaa, Agosti 16 kwa mchezo baina ya Manchester United na Fulham.