Vijana wapewa mchongo

Thursday August 04 2022
mchongo pic
By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Baadhi ya vijana wanaopenda mchezo wa kubet, wameelezea furaha yao baada ya kampuni mpya ya GwalaBet iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam kutoa nafasi moja ya kucheza bure kila siku.

Kampuni hiyo iliyozinduliwa leo Alhamisi Agosti 4, 2022 inakuwa ni ya kwanza kutokea nchini Tanzania kwani hakuna mchezo mwingine unaompa mchezaji nafasi ya kucheza pasipo kuweka dau.

Shilton Ally kutoka Kariakoo alisema amekuwa mdau ya michezo ya kubahatisha kwa miaka mingi, lakini mchezo huo mpya unampa nafasi ya kubashiri bila kuweka dau unamfanya azidi kufurahia betting.

“Mchezo wa kubet ni mzuri na inapofikia wenye makampuni wakatufikiria walaji inakua ni nzuri zaidi, inatoa motisha kama ninaweza kubashiri mpira au mchezo mwingine bila kuweka hela yoyote,” amesema.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Balozi wa GwalaBet, Cedou Mandingo maarufu Babuu wa Kitaa amesema huu ni mchezo unaolenga kumpa fursa ya ushindi kila mchezaji.

“Michezo yote lazima uweke dau la kucheza, lakini GwalaBet tunataka kumpa kila mtu fursa ya kushinda. Kila siku unapoamka unakuwa na nafasi ya kuweka mkeka wako wa bure bila masharti yoyote kisha unasubiri ushindi wako,” alisema Balozi.

Advertisement

Gwala ni neno linalotumika katika mazungumzo ya kawaida hasa baina ya vijana likiwa na maana ya tano au mia tano.

“Kama lilivyo jina lake mchezo huu ni unalenga kuwashirikisha wachezaji wote kama wanafamilia ambapo hata kama huna dau la kucheza unakuwa na nafasi ya kucheza. Baada ya mkeka wa bure unaotolewa kila siku mchezaji anaweza kuweka mwingine kwa dau dogo la kuanzia shilingi mia tano ili kujishindia,” amesema Babuu wa Kitaa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Gwalabet, Lumuliko Mengele amesema Gwala ni kampuni inayomilikiwa na wazawa na inalenga kuhakikisha Watanzania wanafaidika zaidi kupitia  mchezo huu.

“Pamoja na nafasi ya kucheza bure, GwalaBet inatoa ofa na bonasi kibao zikiwemo cashout, multibet hadi asilimia 500, Jackpot kubwa ya Sh200 milioni,” amesema Mengele.

Advertisement