Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya Wakenya Ligi Kuu Bara leo

Muktasari:

  • TRA United inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi moja sawa na Pamba Jiji ambayo inashika nafasi ya 14.

Mwanza. Mechi mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara zinachezwa leo katika viwanja na miji tofauti lakini mvuto unaonekana utakuwepo katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ambako Pamba Jiji itaialika TRA United kuanzia saa 8:00 mchana.

Mchezo huo unakutanisha timu mbili zinazofundishwa na makocha kutoka Kenya ambapo wenyeji Pamba wapo chini ya Francis Baraza huku TRA United wakiwa chini ya Kassim Otieno.

Pamba Jiji haijawa na mwanzo mzuri msimu huu ikitoka sare moja na kupoteza moja huku TRA ikitoka sare katika mechi yake moja.

Baraza amesema anaamini vijana wake wana nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi kesho kutokana na maandalizi waliyofanya.

“Tunapofanya mazoezi unaona morali, jambo ninalosema ni kwamba vijana wangu wabebe kile tunachokifanya mazoezini. Wakileta kwenye mchezo wa kesho bila shaka tunaweza kuondoka na ushindi,” alisema Baraza.

Kocha wa TRA United, Kassim Otieno amesema wametumia wiki moja kujiandaa na mchezo huo na kuwasoma wapinzani wao wanavyocheza, hivyo, wako tayari kupata pointi tatu.

“Kama mechi ya kwanza tulifunga mabao mawili basi mechi ya pili tunaweza pia kuzuia tusifungwe. Kwa hiyo unaweza kuona wiki nzima tumejaribu kuona namna gani tunaweza kuzuia na jinsi ya kufunga mabao. Hivyo tumejiandaa vizuri kuondoka na matokeo chanya,” alisema Otieno.

Mchezo mwingine loe utakuwa baina ya Mtibwa Sugar itakayoialika Fountain Gate katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma kuanzia saa 10:15 jioni.