Wanamichezo wamlilia Mwinyi

Wanamichezo kote nchini wameonyesha masikitiko yao baada ya kutangazwa kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi.

Rais Samia Suluhu Hassan, muda mchache uliopita ameutangazia umma kifo cha Mwinyi ambaye alikuwa maarufu kama Mzee Rukhsa, kilichotokea kwenye Hospitali ya Nzena Jijini Dar es Salaam.

Wanamichezo mbalimbali wameonyesha kusikitisha na kifo hicho, na kutumia kurasa zao kuonyesha masikitiko yao.

Mwingizaji wa filamu, Jimmy Mafufu, ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram: Pumzika kwa Amani Rais wetu wa awamu ya pili, Mzee Mwinyi, umevipiga vita vilivyo vizuri, imani umeilinda, mwendo umeumaliza.

"RIP Mzee Ruksa, ulipostaafu nilikuwa darasa la kwanza lakini simulizi zako nje nilizisikia na zinaishi hadi sasa.

Mwanamuziki Zuwena Mohammed, maarufu kama Shilole, naye ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram,''innallilah'' Wainanillah Rajuin. akisindikiza na picha ya Mwinyi.

Mchambuzi maarufu wa soka Tanzania, Edo Kumwembe yeye ameandika "Pumzika kwa Amani."

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, aliandika Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un, kwaheri muumini, mcha Mungu, mtu muungwana, kiongozi wa watu mzee Mwinyi... kwa maneno yako kitabu chenye hadithi nzuri kimekamilika."

PUMZIKA KWA AMANI MZEE RUKHSA.