Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapiga kura Simba wagoma

Muktasari:

  • Wapiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Simba wamegomea uamuzi wa kamati ya Uchaguzi wakati wa kuchagua wajumbe.

Wapiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Simba wamegomea uamuzi wa kamati ya Uchaguzi wakati wa kuchagua wajumbe.

Kamati hiyo ambayo imeenda kujipanga, ilipofika saa 9.45 mchana ilitoa tamko la kupiga kura kwa mjumbe mmoja kati ya 12 wanaowania nafasi tano, moja ikiwa mwanamke.

Tangazo la kamati limetaka kila mpiga kura kuchagua mjumbe mmoja tu, kisha baadae atakayekuwa na kura nyingi ndiye atakuwa mshindi.

Tangazo hilo liliibua zomea zomea ukumbi mzima wapiga kura wakipaza sauti kuwa hawataki.

Katiba inaruhusu kuchagua wajumbe watano, kwanini tuchague mmoja, hatutaki, ilikuwa ni kauli za wanachama ndani ya ukumbi huo.

Kamati imekwenda chemba kujadiliana upya jambo hilo lililokataliwa na wapiga kura hao.