Wapinzani Simba, Yanga CAFCL hawa hapa

Muktasari:

  • Katika droo hiyo ambayo imechezeshwa leo, jioni huko Misri huku ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF, Samson Adamu, Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuwafahamu wapinzani wake kabla ya Yanga kufuata baadaye.

Dar es Salaam. Hatimaye wapinzani wa Simba na Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wamefahamika ambapo sasa Yanga itavaana na Mamelodi Sundowns ya .

Hii itakuwa mara ya pili kwa Simba kukutana na Al Ahly ndani ya msimu mmoja, ikumbukwe mwanzoni mwa msimu, timu hizo zilikutana kwenye ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League, mchezo wa kwanza Mnyama alitoka sare ya mabao 2-2, kwenye Uwanja wa Mkapa huku walipokwenda Misri wakitoka tena sare ya bao 1-1.

Safari ya Mnyama kwenye michuano hiyo iliishia hapo licha ya matokeo ya jumla kuwa sare ya mabao 3-3, waliondolewa kutokana na idadi kubwa ya mabao ambayo aliruhusu akiwa nyumbani kwa upande wa Yanga mara ya mwisho kukutana na Mamelodi ilikuwa miaka 23 iliyopita ambapo ilikuwa katika raundi ya pili ya michuano hiyo.

Yanga ilishindwa kufua dafu, ikiwa Afrika Kusini ilipoteza kwa mabao 3-2 na ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya mabao 3-3.

Mechi za mkondo wa kwanza zitapigwa kati ya Machi 29-31 na kurudiana kati ya Aprili 5-7, 2024. Simba na Yanga zitaanzia nyumbani kwenye michezo hiyo huku zikiwa na kibarua kizito mbele yao cha kumalizia ugenini.

Wakati Simba na Yanga zikiwa na kazi ya kufanya kwenye hatua hiyo, mechi nyingine za robo fainali ni kati ya TP Mazembe ya DR Congo dhidi ya Petro Atletico na Esperance Sportive de Tunis dhidi ya ASEC Mimosas.


NUSU FAINALI

Esperance/ASEC vs Yanga/Mamelodi

TP Mazembe/Petro Atletico vs Simba/Al Ahly


Upande wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Future itavaana na ndugu zao wa Mirsi, Zamalek, Abu Salim ya Libya itacheza dhidi ya RS Berkane ya Morocco, Rivers United ya Nigeria itakutana na USM Algers ya Algeria huku Stade Malien ya Mali ikipangwa na Dreams FC ya Ghana.


NUSU FAINALI

Rivers United/USM Alger vs Abu Salim/RS Berkane

Future/Zamalek vs Stade Malien/Dreams