Wawa ndio basi tena Simba, apewa Mtibwa

Tuesday June 21 2022
wawapiic
By Leonard Musikula

BAADA ya kuitumikia klabu ya Simba kwa misimu minne, Pascal Wawa hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao ambapo mkataba wake utamalizika mwisho wa mwezi huu huku mchezo wa Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mchezo wake wa mwisho.

Simba imethibitishi kuachana na beki huyo raia wa Ivory Coast aliyejiunga na Simba mwaka 2018 akitokea Azam FC leo Juni 21, 2022.

Pascal Wawa hakuwa na msimu mzuri ukilinganisha na misimu iliyopita huku ujio wa beki Mkongo Enock Inonga ukifanya nafasi yake kuwa finyu ndani ya kikosi cha Simba  mara nyingi akisotea benchi.

Katika kipindi alichokaa kikosini hapo Wawa amekuwa akicheza eneo la safu ya ulinzi akiisaidia na Joash Onyango, Kennedy Juma pamoja na Henoc Inonga.
Wawa ni mchezaji wa tatu kuagwa na Simba baada ya Bernard Morrison pamoja na Rally Bwalya aliyeangwa hivi karibuni.

Advertisement