Yanga kuachana na Bumbuli rasmi

Muktasari:

  • UONGOZIwa klabu ya Yanga umethibitisha rasmi kuachana na aliyekuwa Ofisa Habari na Mkuu wa Idara ya Habari na mawasiliano wa timu hiyo, Hassan Bumbuli.

UONGOZIwa klabu ya Yanga umethibitisha rasmi kuachana na aliyekuwa Ofisa Habari na Mkuu wa Idara ya Habari na mawasiliano wa timu hiyo, Hassan Bumbuli.

Taarifa iliyotolewa leo na klabu hiyo katika ukurasa wake mtandao wa kijamii wa Instagram imethibitisha kumuaga kiongozi huyo aliyeitumikia timu hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Aidha uongozi wa timu hiyo umesema Bumbuli amemaliza mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo ya Wananchi  hivyo wanamshukuru sana kwa kazi nzuri  na kumtakia kila la kheri na mafanikio katika maisha na kazi zake nje ya klabu hiyo.

Kabla ya Bumbuli kuwa Ofisa Habari Yanga alishawahi kufanya kazi kama mhariri kwenye kampuni ya New Habari Corporation.