Yanga mguu mmoja makundi CAF

What you need to know:

  • Yanga imeanza ugenini kwenye raundi hii ya pili huku wenyeji wao, Al Merrikh ya Sudan ikiutumiwa     Uwanja wa Pele, Rwanda kama uwanja wa nyumbani kutokana na mchafuko yaliyopo nchini kwao.

Mabao mawili ya Yanga yaliofungwa na washambuliaji Kennedy Musonda na Clement Mzize dhidi ya ya Al Merrikh yametosha kuitanguliza Yanga mguu mmoja mbele katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imeanza ugenini kwenye raundi hii ya pili huku wenyeji wao, Al Merrikh ya Sudan ikiutumiwa Uwanja wa Pele, Rwanda kama uwanja wa nyumbani kutokana na mchafuko yaliyopo nchini kwao.

Musonda ndiye aliyefungua akaunti ya mabao kwa Yanga baada ya kumalizia kwa kichwa pasi ya Pacome Zouzoua, baada ya Aziz Ki Stephane kufanyiwa faulo na mchezaji wa Al Merrikh jirani na eneo la hatari.

Pasi ya kisigino ya Kiungo Azizi KI imetosha kwa Yanga kupata bao la pili kwa Mzize na mpira kumalizika kwa mabao 2-0
Yanga ilifanya mabadiliko kadhaa kwenye mchezo huo katika kipindi cha pili baada ya milango kuwa migumu katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Miguel Gamondi aliamua kuwaingiza Musonda, Jesus Moloko, Hafidh Konkoni na Zawadi Mauya ambao walionekana kuongeza nguvu kwenye timu.

Huku akiwatoa Mudathir Yahya, Mzize, Azi Ki na Pacome baada ya kupata kile ambacho alihitaji kutoka kwao.

Mechi ya marudiano ya kuitafuta hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itapigwa Septemba 30 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.