Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Simba kuumana Oktoba 10, ratiba ikianikwa hadharani

Muktasari:

  • Ligi Kuu msimu ujao itaanza rasmi, Agosti 14, 2026 kwa michezo mitatu itakayochezwa katika miji na viwanja tofauti.

Dar es Saalam. Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), leo Jumatatu, Julai 20, 2026 imetangaza ratiba ya Ligi Kuu ya NBC msimu ujao wa 2026/2027 ambayo inaonyesha mechi ya kwanza ya Watani wa Jadi, Simba na Yanga itachezwa Oktoba 10, 2026.

Simba watakuwa wenyeji wa mechi hiyo ambayo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, itachezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Kupangwa kwa mechi baina ya timu hizo kuchezwa Oktoba 10, 2026, kutafanya timu hizo zikutane mara sita ndani ya mwaka huu.

Tayari zimekutana katika mechi mbili za Ligi Kuu msimu uliopita, zikakutana katika mechi moja ya Kombe la Muungano, zitakutana katika mechi ya Ngao ya Jamii, Agosti 12, 2026 na kisha hiyo ya mzunguko wa kwanza ya msimu ujao.

Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo umepangwa kuchezwa Februari 6, 2027 ambao Yanga itakuwa mwenyeji katika Uwanja wa Uhuru.

Ligi Kuu msimu ujao itaanza rasmi, Agosti 14, 2026 kwa michezo mitatu itakayochezwa katika miji na viwanja tofauti.

Mechi ya kwanza itakuwa katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza baina ya wenyeji Pamba Jiji dhidi ya Dodoma Jiji kuanzia saa 8:00 mchana.

Baada ya hapo, Mbeya City itaikaribisha Geita Gold katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya kuanzia saa 10:15 jioni.

Mchezo wa mwisho kwa siku hiyo utakuwa baina ya Singida Black Stars dhidi ya Fountain Gate kuanzia saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Airtel, Singida.