Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Simba mguu sawa, CAF yapuliza kipyenga

Muktasari:

  • Mashindano ya CAFTanzania itawakilishwa na Yanga na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam na Singida Black Stars zikiwakilisha katika Kombe la Shirikisho.

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza rasmi kalenda ya mechi za msimu wa 2026/27 wa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika mashindano hayo Tanzania itawakilishwa na Yanga na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam na Singida Black Stars zikiwakilisha katika Kombe la Shirikisho.

Msimu uliopita klabu hizo ziliweka rekodi kwa zote nne kuvuka kucheza hatua ya makundi ya mashindano hayo, lakini zilishindwa kufuzu kwa hatua robo fainali.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, msimu wa 2026/27 utaanza kwa hatua ya kwanza ya mchujo, ambapo mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa kati ya Septemba 4 hadi 6, 2026, huku marudi-ano yakifanyika Septemba 11 hadi Septemba 13 mwaka huu.

Hatua ya pili ya mchujo itaanza kwa mechi za mkondo wa kwanza kati ya Oktoba 16 na Oktoba 18 maaka huu na mechi za marudiano zitachewa Oktoba 23 hadi 25, 2026.

Baada ya hatua za mchujo kukamilika, hatua ya makundi ya mashindano yote mawili itaanza mwishoni mwa mwezi Novemba 2026.


Ratiba ya hatua za mchujo

Hatua ya kwanza (Mkondo wa kwanza), Septemba 4–6  2026

Hatua ya kwanza (Marudiano) Septemba 11 hadi 13, 2026

Hatua ya pili (Mkondo wa kwanza) Oktoba 16– Oktoba 18, 2026

Hatua ya pili (Marudiano), Oktoba 23–25, 2026


Ratiba ya hatua ya makundi

Mzunguko wa kwanza ni Novemba 27–29, 2026


Mzunguko wa Pili ni Desemba 4–6, 2026

Mzunguko wa tatu, Desemba 18–20, 2026

Mzunguko wa nne ni Januari 8–10, 2027

Mzunguko wa tano ni Januari 15–17, 2027

Mzunguko wa sita ni Januari 22–24, 2027


Ratiba ya hatua za mtoano

Robo fainali (Mkondo wa kwanza), Februari 26–28, 2027

Robo fainali (Marudiano), Machi 5–7, 2027

Nusu fainali (Mkondo wa kwanza), Aprili 9–11,  2027

Nusu fainali (Marudiano), Aprj 16–18, 2027

Fainali itachezwa kati ya Mei Mei na 31, 2027, kulingana na ratiba itakayothibitishwa na CAF baadaye.