Yanga yaendelea kutupia moja

Sunday October 10 2021
yaga pic
By Charity James

BAO pekee lililofungwa kipindi cha kwanza na Fiston Mayele limetosha kuwapa ushindi Yanga wa 1-0 dhidi ya JKU ya Zanzinar katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Makapa jijini Dar es Salaa.

Pamoja na Yanga kufanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa Deus Kaseke, David Bryson, na Dickson Ambundu na nafasi zao kuchukuliwa na Makambo, Ditram Nchimbi na Adeyum hayakuwa na madhara kwa wapinzani.

mayele pic

Kipindi cha pili Yanga waliendeleza mashambulizi dakika ya 52 Mayele akiwa na kipa alishindwa kutumia nafasi hiyo kwa kupiga shuti mkaa ambalo lilinyakuliwa na kipa wa JKU.

Mbali na nafasi hiyo pia Makambo alitengewa mipira dakika ya 55 na 78 zote alishindwa kuzituma na kushindwa kuisaidia timu yake kuongeza bao.

Pamoja na kukosa nafasi Yanga imeonyesha kucheza mpira mzuri wakiwanyima nafasi wapinzani wao kufanya mashambulizi.

Advertisement

Dakika ya 73 JKU walipiga shuti langoni kwa Yanga ambalo lilinyakuliwa na kipa Johora ambaye hajapata kashikashi nyingi langoni kwake kutokana na uimara wa safu yake ya ulinzi.

Advertisement