Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yakwea kileleni Ligi Kuu

Muktasari:

  • Hata hivyo KMC imeendelea kuwa na wakati mgumu ikiwa mkiani kwenye ligi baada ya kucheza michezo sita na kufanikiwa kushinda mmoja tu hadi sasa.

Dar es Salaam. Yanga imekwea kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya KMC katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Huu ndiyo mchezo ambao umezalisha mabao mengi kwenye ligi msimu huu hadi sasa baada ya mechi nyingi kuishia idadi ya mabao matatu.

Ushindi huu umeifanya Yanga ifikishe pointi 10 ikiwa ni moja mbele ya Simba ambayo ina pointi tisa lakini ikiwa mchezo mmoja pungufu.

Kipindi cha kwanza kilikuwa bora kwa timu zote zilikionyesha kiwango kizuri ambapo kilimalizika kwa sare ya bao 1-1, lakini cha pili kilikuwa upande wa Yanga zaidi ambapo ilifanikiwa kufunga mabao matatu kwenye dakika 45 za mwisho.

Yanga imefunga mabao yake kupitia kwa Maxi Nzegeli, Pacome Zouazoa na Andy Boyeli ambaye amefanikiwa kufunga mabao mawili kwenye mchezo huo yakiwa ni ya kwanza kwake kwenye ligi tangu alipotua nchini mwanzoni mwa msimu huu.

Bao pekee la KMC liliwekwa kimiani na Daruwesh Saliboko kipindi cha kwanza cha mchezo huo likiwa ni bao la pili timu hiyo inafunga msimu huu.

Hata hivyo KMC imeendelea kuwa na wakati mgumu ikiwa mkiani kwenye ligi baada ya kucheza michezo sita na kufanikiwa kushinda mmoja tu hadi sasa.