Yondani uso kwa uso na Fiston

Wakati wenyeji Polisi Tanzania wakibakiza dakika chache kuwakaribisha Yanga kocha wao Malale Hamsini amefanya mabadiliko matatu katika kikosi chake.

Malale ameendelea kuuamini ukuta wake ulimaliza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC akianza na kipa  Mohammed Yusuf, Deodatus Peter, Juma Ramadhan, mabeki wa kati wakiwa Iddy Mobby na Kelvin Yondani ambapo beki huyo atakuwa akikutana kwa mara ya kwanza ana timu yake ya zamani walioshindwana kuongeza mkataba.

Katika kiungo Malale amemrudisha nahodha wake Pato Ngonyani ambaye alipumzishwa mchezo uliopita akichukua nafasi ya Abdulaziz Makame ambaye hataweza kucheza mchezo huu kufuatia kuwa kwa mkopo unaomzuia kucheza katika timu yake ya zamani.

Pato ambaye ni nahodha wa Polisi atakuwa sambamba na Nassoro Maulid na Marcelo Kaheza katika eneo la kiungo.

Safu ya ushambuliaji Malale amemweka benchi mshambuliaji wake Gerrald Mathias aliyefunga bao pekee katika mchezo uliopita dhidi ya KMC huku nafasi yake ikichukuliwa na Kassim Shaban.

Wengine katika safu hiyo ni pamoja na Daruesh Saliboko na Tariq Seif ambaye msimu uliopita pia aliitumikia Yanga.

Kwenye benchi la Polisi wako kipa Msafiri Mkumbo, Shaban Stambuli, Yahaya Mbegu, Deusdedity Cosmas, Mohammed Kassim, Pius Buswita na Mathias