Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zubimendi, Gyokeres wang'aa Arsenal ikiichapa Nottingham Forest

Muktasari:

  • Gyokeres alisajiliwa na Arsenal katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwaka huu na hadi saa ameshaifungia timu hiyo mabao matatu katika Ligi Kuu England (EPL).

Arsenal imerudi katika mstari wa ushindi baada ya leo kutumia vyema Uwanja wake wa nyumbani wa Emirates, London kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nottingham Forest.

Timu hiyo ambayo ilipoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Liverpool, leo imejiuliza na kupata ushindi huo wa mabao matatu yaliyofungwa na Viktor Gyokeres na Martin Zubimendi.

Zubimendi ndiye alianza kuifungia Arsenal bao katika dakika ya 32 akimalizia kwa shuti kali mpira ambao uliokolewa langoni mwa Nottingham Forest baada ya krosi ya Noni Madueke.

Hilo limekuwa ni bao la kwanza kwa kiungo huyo kuifungia Arsenal kwenye EPL tangu alipojiunga nayo msimu huu akitokea Real Sociedad na lilidumu hadi muda wa mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa Arsenal kupata bao la pili kupitia kwa Viktor Gyokeres akimalizia pasi ya Eberechi Eze.

Kwa Gyokeres, bao hilo ni la tatu kwake kwenye Ligi Kuu ya England na anaongoza chati ya kufuania nyavu akiwa sawa na Erling Haaland wa Manchester City.

Arsenal ilipata bao la tatu katika dakika ya 79 kupitia kwa Zubimendi tena baada ya kiungo huyo kumalizia kwa kichwa krosi ya Leandro Trossard.

Ushindi huo umeifanya Arsenal kufikisha pointi tisa na hivyo kukaa kileleni mwa msimamo wa EPL ikizipiku Liverpool yenye pointi tisa kama hizo na Chelsea yenye pointi saba lakini zenyewe zina michezo pungufu ambapo kila moja imecheza mechi tatu huku Arsenal ikicheza nne.

Hata hivyo furaha ya Arsenal kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi inaweza kuwa ya muda kwani watajikuta wanashushwa iwapo Chelsea itaibuka na ushindi dhidi ya Brentford katika mchezo ambao utaanza saa 4:00 usiku.

Katika mchezo wa leo, refa Darren England aliwaonyesha kadi za njano, Riccardo Calafiori wa Arsenal na Neco Williams wa Nottingham Forest kutokana na faulo walizocheza kwa wachezaji wa timu pinzani.