Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameshiriki ibada fupi ya kuaga mwili wa Suezi Dani Maradufu, aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, leo Ijumaa, Julai 3, 2026 katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma.
Mwili wa Suezi umeagwa Kigoma na unatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Tarime.