Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na mkewe mama Mbonimpaye leo Agosti 4, 2024 wamesafiri kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam kwa usafiri wa treni ya kisasa ya umeme inayotumia reli ya SGR. Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la klabu ya Yanga la kilele cha Wiki ya Mwananchi linalofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa leo. Picha na OMR